ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.
Diamond asitisha kuachia wimbo mpya, yadaiwa kisa Alikiba
Muimbaji Diamond Platnumz wiki hii baada ya kuachia nyimbo mbili,
Sikomi na Niache, aliahidi Ijumaa hii kuachia rasmi wimbo wake mpya
uitwao ‘Waka’.
Meneja wa muimbaji huyo, Sallam amewaomba radhi mashabiki wa muimbaji huyo mwenye tuzo nyingi za kimataifa kwa madai kuna dharura imetokea hivyo atashindwa kuachia project hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa muziki.
“Tunaomba msamaha wimbo wa ‘Waka’ ulitakuwa kutoka siku ya leo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu kwahiyo hautaweza kutoka leo lakini muda sio mrefu tutawajuza!! Sorry for any inconvenience,” aliandika meneja huyo.
Wadau wa mambo wamedai muimbaji huyo ameshindwa kuachia kazi hiyo mpya ili kuepusha kazi hiyo kushindanishwa na wimbo mpya wa msanii wa RockStar4000, Alikiba, ‘Maumivu Per Day’.
Hata hivyo mashabiki wa Diamond wameonyesha kuchukizwa vikali na uamuzi huo huku wengine wakiwa na maoni tofauti.
Haya ni maoni ya baadhi ya mashabiki hao.
jacky_nchimbi_tz
Daaaaaah big boss tulishaweka mabando ye2 ya kutosha 😂😂😂😂😂😂, ila co mby we are waiting for that ngasalah_platnumzivyo ivyo mzee wanajidai wanaakil kuliko cc wapumbavu tumewaweza watembelea nyota tusiachie ataikiwezekana wiki nzima.
prosper_iam
Sasa boss mendez mbona unazingua????si wenzenu tumetoa nyimbo mbili na video juu maan tulitegemea ikitoka hii ya simba leo tungepata boost ya kutosha kupitia mgongo wa chibu sa umepostpone ngoma ya mond na rozeey si mashabiki wa kiba tutafanyaje jmniii😥😥😥😥 mbn mjini patakua pachungu hii wiki jmn..
janechalz
Tunausubiri kwa hamu ila usiwe wa kuchambua wanawake wake hakuna mwanaume asie acha na kuachwa yanayotokea kwake ni kama kwa diamond yanaqatokea wanaume wengi sio kika nyimbo zari ,tako la wema kahonga gari abadilike kweli tunaitaji nyimbo za mapenzi zenye kumpa funzo kila asikiaye @bravesty_sk huo wakawaka utakuwa wa kimataifa ZAID HAKUNA WEMA WALA ZARI MBONA WOTE WANAUME WANATOMBA JAMANI!! HAWAWANYANYAMBUI WAPENZI WAO ILA YEYE MOND NAMPENDA SANA ILA ABADILIKE
festontan
Safi sana walitaka watembele nyota ya simba mwacheni li wimbo lake libume halafu anazuga eti huo wimbo ni unofficial wakati ameuachia special, ingekuwa ameachia kipande nusu ndio angeandika unofficial sasa wimbo mzima unaitaje unofficial, Nyau kabisa Mendez una akili sana #WAKAWAKA# ndio habari ya mjini imekula kwake @sallam_sk
SOURCE;BONGO5

BREAK NEWS...Diamond Platnumz aahirisha kuachia kolabo yake na Rick Ross
Uongozi msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz umeahirisha kuachia wimbo mpya wa msanii huyo ‘Waka’ ambao amemshirikisha rapper kutoka nchini Marekani Rick Ross.
Rick Ross katikati, Diamond Platnumz kulia na meneja wake Babu Tale wakati wa kushoot video ya WAKA mapema mwezi Oktoba mwaka huu.
Akithibitisha hilo Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam amesema kuwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao wimbo huo hauwezi kutoka leo Desemba mosi kama ilivyokuwa imepangwa awali.
“Tunaomba Msamaha Wimbo wa #Waka ulitakuwa kutoka siku ya leo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu kwahiyo hautaweza kutoka leo lakini muda sio mrefu tutawajuza!! Sorry for any inconvenience“ameandika Sallam kwenye ukurasa wake wa Instagram.
SOURCE;BONGO5
Wachina 5 wakamatwa na magamba 652 ya kakakuona
RAIA watano wenye asili ya China wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma baada ya kupatikana na nyara za serikali kinyume cha sheria.
Watuhumiwa hao walipatikana wakiwa na magamba 652 ya kakakuona na kucha tano kakakuona, kucha nne za simba na jino moja la simba. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Gilles Muruto akizungumza na vyombo vya habari jana, alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika Kiwanda cha Kusaga Kokoto cha Kampuni ya Sands Industries Limited kilichopo katika Kijiji cha Mpamantwa wilayani Bahi mkoani Dodoma.
Kamanda Muruto alisema watu hao walikamatwa Septemba 11, mwaka huu kwa ushirikiano baina ya Polisi Dodoma na askari wa Kikosi cha Kupambana Dhidi ya Ujangili (KDU) Kanda ya Kati, Manyoni. Kamanda Muruto alisema uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini mtandao wa ujangili na wa wageni wanaoingia nchini ambao wanajihusisha na uhalifu wa aina mbalimbali.
Upelelezi ukikamilika watafikiwa mahakamani kwa mujibu wa sheria. Katika tukio lingine, Kamanda Muroto alisema katika msako unaoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Dodoma, wamewakamata watuhumiwa 12 wa makosa ya kuvunja na kuiba vitu mbalimbali. Alisema licha ya kukamata watuhumiwa hao, pia jeshi hilo limeokoa mali zilizoibwa kutokana na uvunjaji wa nyumba za watu mbalimbali. Alizitaja mali hizo waliokamata kuwa ni televisheni zenye kioo bapa (13), redio sabwoofer mbili, spika tano na deki moja, printa ya kompyuta moja, busta ya gari moja na bhangi kete 12.
Kamanda wa Polisi, Muroto aliwaka wale wote ambao wameibiwa vifaa hivyo katika maeneo mbalimbali wafike Polisi Dodoma ili uzitambua mali zao. Alisema kati ya watuhumiwa hao waliokamatwa ni Dotto Kapenga (43), mkazi wa Chang’ombe, mjini Dodoma ambaye alikamatwa na sare za jeshi zikiwamo kombati, suruali moja, sweta mbili, mikanda mitatu, kofia tano, buti pea moja vyote mali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Alisema mtuhumiwa huyo pia alikamatwa na koti la mvua na cheo cha luteni ussu ambacho ni cheo kinachomtambulisha askari mwenye nyota moja. “Uporaji wa mali za watu kwa kutumia pikipiki na unyang’anyi wa pikipiki, umepungua hasa baada ya kuwakamata watuhumiwa halisi na kuwafikisha mahakamani. Kamanda Muroto aliwataka wananchi waendelee kutoa taarifa za wahalifu kwa Jeshi la Polisi na wao watazifanyia kazi kwa ukamilifu. CHANZO HABARI LEO
Polisi yaua mratibu Wadau wa mauaji ya Kibiti
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam wamemuua mtuhumiwa wa ujambazi, Anaf Kapela anayedaiwa kuwa mratibu wa matukio ya mauaji Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani.
Pia inadaiwa alikuwa ni mmoja wahusika wa matukio mbalimbali ya kijambazi ikiwemo kuvamia mabenki na kuua askari wanane wa wilaya ya Kibiti. Kapela pia anadaiwa kuhusika na mauaji ya Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Newala mwaka 2013, uvamizi wa kituo cha polisi Stakishari mwaka 2015, kuuwa askari watatu na kupora silaha mbili aina ya SMG kwenye benki ya CRDB Mbande mwaka 2016, na pia kuvamia benki ya Access Mbagala pamoja na benki ya NMB Mkuranga.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Lazaro Mambosasa alisema tukio hilo lilitokea Septemba 12 maeneo ya Kivule Chanika. “Mtuhumiwa huyu ndiye aliyekuwa kiongozi na mratibu mkuu wa matukio hayo Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani na ametaja wahusika alioshirikiana nao katika matukio yaliyotajwa, hivyo ufuatiliaji bado unaendelea,” alisema Mambosasa.
Alisema kabla ya tukio hilo askari walipokea taarifa ya kuwepo kwa mtu huyo maeneo hayo na kuweka mtego na kufanikiwa kumkamata mtu huyo baada ya kumjeruhi kwa risasi ya goti la mguu wa kulia na mkono wa kushoto wakati akijaribu kukimbia. Aliongeza kuwa jambazi hilo lilifika maeneo hayo ya Kivule kwa ajili ya kuuguza majeraha ya risasi aliyopigwa ambapo alikuwa anatibiwa na bibi mmoja baada ya kukimbia operesheni ya Kibiti.
“Askari wetu waliweka mtego muda wa saa nne usiku na kuzingira nyumba aliyokuwa akipatiwa matibabu, lakini badala yake alitokea nyumba nyingine alipoona askari alianza kukimbia ndipo alipigwa risasi kwenye goti la kulia, begani chini ya mkono wa kushoto,” alisema Mambosasa. Mambosasa alisema baada ya upekuzi mtuhumiwa huyo aligundulika kuwa na makovu makubwa matatu ya risasi sehemu mbalimbali ikiwemo shavu la kulia, bega la kulia na mguu na ndiyo alikuwa akipata matibabu hayo. CHANZO HABARI LEO
Wabunge kuondoa umri wa kuwania urais Uganda
Wabunge kutoka chama kinachotawala nchini Uganda NRM wamekubaliana kuwasilisha mswada ambao unapendekeza kuondewa miaka ya kuwania urais nchini Uganda.
Ikiwa watafaulu mswada huo utamwezesha Rais Yoweri Museveni ambaye anaaminika kuwa mwenye umri wa miaka 73, kuwania tena uchaguzi wa mwaka 2021.
Amekuwa madarakani tangu mwaka 1986 na kwa sasa anahudumu muhula wake wa tano madarakani.
Mswada ambao huo amabo unaungwa mkono na wabunge 200 wa NRM unataka kukifanyia mabadiliko kipengee cha 102 (b) cha katiba ya Uganda, ambacho kinaweka umri ambao mtu anaweza kuwania urais wa kati ya miaka 35 na 75
Wengi wanasema kuwa NRM ambacho kina wabunge wengi, kitasababisha mabadiliko ya katiba lakini wengibe ndni ya NRM waekana.
Wabunge wanasema kuwa watawasilisha mswada huo bungeni katika kipindi cha wiki moja.
Uturuki yanunua mfumo wa kujilinda na makombora kutoka kwa Urusi
Uturuki imetia saini makubaliano yaliogubikwa na utata na Urusi kulihami jeshi lake na mfumo wa kudungua makombora wa S-400.
Rais Reccep Tayyip Erdogan alisema kwamba Ankara tayari imetoa malipo ya kwanza ya mkataba huo unaotarajiwa kugharimu $2.5b.
Uturuki ina jeshi la pili kwa ukubwa katika muungano wa NATO.
Washirika wa muungano huo wa majeshi ya kimataifa wametakiwa kununua mifumo ya hali ya juu ya kujilinda dhidi ya makombora.
Uturuki imekuwa ikiimarisha uhusiano na Urusi baada ya ushirikiano wake na Marekani kuzorota.
Urusi inasema kuwa mfumo huo wa kujilinda dhidi ya makombora unaweza kubaini kombora lililopo umbali wa kilomita 400 na unaweza kudengua hadi makombora 80 kwa mpigo, ukilenga makombora mawili kila awamu.
Uturuki imekuwa ikipinga mpango wa Marekani kuwaunga waasi wa Kikurdi nchini Syria ambao wanahusishwa na waasi wa kikurdi nchini Uturuki.
Urusi iliweka mfumo huo karibu na kambi yake ya kijeshi katika eneo la Latakia nchini Syria mnamo mwezi Disemba 2015 baada ya ndege ya kijeshi ya Uturuki kudengua nedege ya kijeshi ya Urusi Su-24 katika mpaka wa Uturuki na Syria.
Kisa hicho kilisababisha mzozo wa kidiplomasia kati ya Urusi na Uturuki, lakini rais Erdogan baadaye alisitisha mgogoro wake na rais Vladmir Putin.
- Mshauri wa kijeshi wa rais Putin, Vladmir Kozhin alisema kuwa makubaliano hayo na Uturuki yanatokana na maslahi ya Urusi.
''Unaweza kuelewa hali ilivyo ambapo baadhi ya mataifa ya magharibi yamekuwa yakiitishia Uturuki''.
Spika wa Bunge kapokea barua ya Prof. Lipumba kufukuza Wabunge 8 CUF
Uamuzi wa Prof. Lipumba umekuja baada ya kuwatuhumu Wabunge na Madiwani hao kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kinidhamu, kukihujumu chama, Kumkashifu na kumdhalilisha Mwenyekiti.
“Nikiondoka hakuna atakayekuwa kama mimi” – kauli 7 za Rais JPM Singida leo
Nimekusogezea mambo 7 makubwa kati ya mengi aliyozungumza kwenye hotuba yake.
‘Pengine nikiondoka mimi hakuna atakayekuwa kama mimi, nasafisha njia ya Rais atakayekuja baada ya mimi’ – Rais @MagufuliJP
‘Ni lazima niyatapike yote haya, nikikaa nayo nitapata presha bure, ila wale walioyafanya wakumbuke na madhambi yao’ – Rais @MagufuliJP
‘Suala la ubinafsishaji mimi silipendi kabisa, siwezi nikawalaumu waliofanya hivyo lakini pia siwezi nikaacha kusema’ – Rais @MagufuliJP
‘Nataka Tanzania hii iwe kama Ulaya na tutafika tu, lakini ili tufike huko ni lazima tutabanana kweli kweli’- Rais @MagufuliJP
‘Wananchi waliojenga kwenye hifadhi ya reli waanze kujiandaa kisaikolojia, wanaweza tu kuanza kubomoa taratibu nyumba zao’- Rais @MagufuliJP
‘Niliporudishwa wizara ya ujenzi nilimfukuza Chief Executive Officer ndani ya siku 3 kwa sababu ya matumizi mabaya ya fedha’ – @MagufuliJP
CHANZO MILLARD AYOWengine mmewachagua lakini wanaongelea ya mambo Dar es salaam tu kosea kuoa unaweza kutoa talaka lakini usikosee kuchagua – Rais @MagufuliJP
Subscribe to:
Posts (Atom)