Video Information
Habari za mchana msomaji natumai
u mzima wa afya
kama kawaida yangu leo nawaletea
pishi nililoandaa kwa
ajili yenu.kama tujuavyo
kila mtu ana namna ya mbalimbali ya
mapishi na jinsi ya
kuandaa chakula.chakula change
cha leo nitakupikia
ugali wa muhoga na mchemsho
wa kuku bili kusahau
kisamvu ambacho kimechanganywa karanga
na nazi.
Ugali wa
muhogo unaliwa sana na
makabila mengi lakini
tumeona kabila
la waha kutoka Kigoma ndiyo asili
yao.moja kwa moja tukaanze kuandaa
mchemsho wa kuku.
MAHITAJI
Kuku wa
kienyeji
Limao
Vitunguu
Pilipili
Tangawizi
Chumvi
Kisamvu kilichochemshwa
Karanga
iliyosagwa
Nazi
Unga wa
muhogo
Moja kwa
moja tunaanza kumchemsha
kuku wetu nitamuandaa kwa kumkata kata
vipande kisha namuweka
katika sufuria.kama tujuavyo
kuku lazima akichemshwa
lazima awekwe tangawizi ingawa
kunasbaadhi ya watu
hawapendi lakini ni
vizuri ukaweka tangawizi
kwa sababu ni
kiungo ambacho kinasaidia
sana kuleta hamu
ya kula unaweza
ukamla kuku mzima
peke yako hahahahahahahahahahhah(natania).pia tangawizi
utaweka ambayo tayari
imetwangwa na siyo ya kusaga
baada ya
hapo unaweka maji
na chumvi kiasi
Kuku wa
kienyeji ni mgumu
sana hivyo lazima
uhakikishe kaiva vizuri
hatua ya mwisho
unamuweka limao na
pilipili alafu unafunukuka
kwa dakika 15
kumbuka uwingi wa
pilipili unatokana ulaji wako
pia unaweza kuweka viazi a ndizi
baada ya hapo ipua
mboga yako itakuwa
tayari unaweza ukainywa
kama supu. Kwa wale wenye waume wanaokunywa
pombe unaweza ukamwandalia
akanywa badala ya
kwenda baa akanywa
kwa raha zake.
Baada
ya hapo
ntaenda kukuandalia kisamvu, nitaanza kwa
kukichemsha kisamvu changu
kwa saa nzima
baada ya hapo ipua
kitakuwa tayari kwa
kuunga anza kwa kubandika
sufurua jikoni kisha
weka vitunguu vikibadilika
rangi na kuwa
kahawia weka kisamvu
chako na uache
vichemke kwa sekunde
kadhaa, baada ya hapo
weka tui la
nazi ambapo unatakiwa
ukoroge taratibu ililishikane
vizuri na mboga
alafu unamalizia kwa
kuwaka karanga baada
ya hapo utaacha
vichemke mpaka ile
harufu ya ubichi
itoke kabisa. Kisamvu chako kitakuwa
tayari kupakuliwa na
kuwekwa mezani.
Tunamalizia
kwa kuandaa ugali
wa muogo jamani
wasomaji wangu kama
tujuavyo ugali wa
muhogo unapikwa tofauti
na ugali wa
kawaida, ugali huu unaanza kwa
kubandika sufuria jikoni
na kuweka maji
kiasi baada ya
kuchemka maji hayo
utaweka unga kiasi
ambao utasongea ugali
wako lakini usikoroge
funika kwa dakika
chache kisha uanze
kusonga utaona kama unavutika
yani hauna desturi ya kuachana kama
ugali wa sembe
hivyo usiache kusonga mpaka
utakapo hakikisha kuwa
unga wote umegusa maji kumaanisha
hauna mabuja utatumia
kama dakika kumi kuwa
tayari.Chakula hiki kinalika na
rika lolote kumaanisha
mtoto hata mtumzima.