Video Information
Malkia
wa filamu Wema Sepetu amewatolea uvivu mashabiki wake katika mitandao ya
kijamii baada ya kuzushiwa kwamba anatoka kimapenzi na kijana huyu katika picha
hapo chini.
Mwigizaji huyo amekanusha uvumi huo na kudai kijana huyo anayesemwa alifanya naye kazi wiki chache zilizopita.
Mwigizaji huyo amekanusha uvumi huo na kudai kijana huyo anayesemwa alifanya naye kazi wiki chache zilizopita.
Kupitia
instgram, Wema ameandika
“Soooooooo,
rumor has it that huyu mkaka ndo new baby, maskini ya Mungu. First &
foremost, nimeongea nae kwa simu akaniomba niweze kuwa MC and special
appearance at his birthday party… I got my paycheck and did my work. Sasa
sielewi mipuuzi na mi***** inayotokwa mapovu kutwaa kunifatilia na maisha yangu
. Ndo mimi nasemaje lets just assume it was true, ni maisha yangu ryt. So i
dont know where all these bia**** with low lives wanakuja na kuanza kufatilia
wats goin on in my Life. Nimewakosea nini Mungu wangu, maisha yangu yamekuwa ni
deal kwenu. Naongea na wewe unaeuza nchi za waarabu…. Leave me and my Life
alone… I keep saying this jamani, Sijawahi bother na maisha ya mtu… I do my
shit…. Huyu kaka simjui na nimemjua on da nyt of his Birthday…. Hata kumuwish
sijamuwish…. Nimewish mtu mwingine Birthday ila mijitu mifala inatokwa
mapovu….. Sasa labda niseme hivi, Wema ana maisha yake nd anaishi atakavyo yeye…
Maisha ya Wema hayamuhusu mtu yoyote mwingine….. And again, My heart belongs to
someone else…. Nd I love my baby tooo much…. So mkiwa mnaandika vitu vyenu vya
kipuuzi…. Again Im talking to you, Stupid Bi-polar Biatch…. Uwe una uhakika…..
Kwani unachotaka kwangu ni nini Mbwa wewe… Wallahy never have I done this in my
Life, But this has just pushed my buttons to da extent that I cannot take it
anymore…. Nimekaa kimya muda mrefu sana and I aint a person dat talks too much…
Ila napigiwa simu nyingi mpaka za demu wake na huyu Ally akilalamika and I had
to do this…. I keep telling you unatia huruma, You need a Hug… But nat from me
honey… Waarabu siku hizi hawalipi nini…? Usiharibie watu bwaana… Afu ni sababu
nilikukataa kuwa karibu na mimi ndo maana umenikaa rohoni au…. Maana nakuskia
tu unaongeeaaa utasema u r my Mom…. Leave me the Fuck alone…!!! una bahati sana
nina wisdom ila leo ningekutukana mbwa wewe… But naaaaaah I got my siblings
tena wadogo goin thru my page so I wouldnt want them to see things they shudnt….
But wewe Nyau… Kuna kitu unachokitafuta kwangu and utakipata soon…. If it wasnt
for my baby nisingefanya huu upuuzi But My baby comes first…. I had to do this”
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Rapa kutoka kundi la East Coast, King Crazy GK ameamua
kuingia Studio kwa Alonem ambapo amebadili maudhui ya uimbaji wake kutoka kurap
na kufanya muziki wa kuimba huku video akiifanya na muongozaji Donald kutoka
Uganda.
, GK amesema kuwa ushindani uliopo kwenye game la
muziki tofauti na zamani ikiwa ushindani ulikuwa wa hapa tu nchini, Ila kwa
sasa wameongezeka wasanii mbalimbali wanaotoka hata nje ya nchi ya Tanzania.
“Nimeamua kuimba lakini ni kutokana na game la Tanzania
kubadilika, zamani tulikuwa tukishindana sisi wa Tanzania kama Juma Nature, AY
na wengine lakini kwa sasa muziki wa Bongo ume’change’ na kuingia mpaka wakina
Wizkind, so kubadilika muhimu” amesema GK.
Hata hivyo GK amebadilisha kabisa aina ya muziki wake
na kutengeneza ngoma yenye mahadhi tofauti kabisa na muziki wake huku mwenyewe
akisema anaandaa mashambulizi makali ili kupambana na game la sasa.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Muigizaji wa vichekesho kwenye tasnia ya filamu nchini,
Salma Jabu a.k.a Nisha Bebee amesherehekea siku yake ya kuzaliwa tarehe 28 kwa
kuamua kutembelea Hospital ya Ocean Road kuwaona wagonjwa waliolazwa katika
hospital hiyo.
Nisha ambaye alisema maisha yake kwa sasa ameamu
kuyaelekeza kwa kusaidia watu na siyo kutafuta skendo kama maisha yake ya
zamani yalivyo kuwa.
“Siku hizi natumia muda mwingi kusaidia watoto yatima
na wagonjwa kwa kuwa nimeamua kuachana na skendo na hata watu ninaokuwa nao
mara nyingi ni watu ambao hawapendi skendo tofauti na wale wa awali kwani
walikuwa wanavujisha siri zangu” Alisema Nisha.
Pia mwanadada Nisha alitumia fursa hiyo kuwasaidia mahitaji
yao ya matibabu na mahitaji madogo madogo ili mradi tu kuhakikisha anamalizia
siku yake ya kuzaliwa na wagonjwa ambapo aliamua kujumuika nao katika siku yake
hiyo.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Studio ambayo imeshawahi kufanya hit song mbalimbali
ikiwemo ya “Siyo Mchoyo” ya Young D na ngoma kibao, Kiri Records imesemekana
kushindwa kulipa kodi ya nyumba ambapo ndipo studio hizo zilipo.
, Rash Doni, ili kufahamu ukweli wa madai hayo ambapo
amesema hajawahi kushindwa kulipa kodi kwenye studio hiyo mbali na yeye kuamua
kuihamishia studio hiyo upande wa pili ili kuongeza ukubwa.
“Sijashindwa kulipia kodi tumeamua kuhamia upande wa
pili ili kupanua studio na wasanii wafurahie mazingira ya studio yetu” Alisema
Rash Doni.
Mbali na madai hayo, Rash Doni alizidi kusema kuwa
wanahama hapo huku bado kodi waliyo lipa ikiwa haijaisha hivyo bado hawawezi
kuwa wana dalili ya kuelekea kudaiwa au kupewa “notice” ya kuhama.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Msanii
wa muziki wa Singeli, Sholo Mwamba amedai muda si mrefu atakuja na collabo zake
na mastaa kadhaa wa muziki wa Bongo Fleva.
Muimbaji
huyo amepata umaarufu zaidi baada ya kushirikishwa na Professor Jay kwenye
wimbo ‘Kazi Kazi’.
Mfalme
huyo wa Singeli amekiambia kuwa tayari wameshamaliza maongezi na Pam Dee pamoja
na Baba Levo na sasa kinachosubiriwa ni kufanya collabo.
Aidha
ameongeza kuwa mashabiki wake wakae tayari kwani kuna vingi vizuri vinakuja
kutoka kwake ukiwemo wimbo ambao atafanya collabo na Bill Nass na mwingine na
Diamond.
Wakati
huo huo, amefafanua kuwa hana ugomvi na msanii mwenzake Man Fongo kwa kuwa yeye
ndio aliyemfundisha kazi wakati huo akiwa kama Dj wake kwahiyo hachukii
mafanikio anayoendelea kuyapata kwenye muziki huo.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Style ya maisha ya
mastaa wengi ulimwenguni inafanana lakini zaidi ni ile tabia yao ya kubadilisha
usiku kuwa mchana kwa sababu mbalimbali, Juma3tata linakuondolea utata.
Siyo jambo la
ajabu kwa mastaa kufanya kazi zao mpaka usiku mwingi kisha alfajiri kulala hadi
mchana wa jua kali, muda ambao watu wengine huwa makazini wakitafuta riziki
zao.
Ukiacha wanaofanya
kazi nyakati za usiku, wapo wengine wanaokuwa kwenye majumba ya starehe, wakila
bata usiku mzima, kisha kutumia mchana kupumzika.
Juma3tata lina
ripoti iliyoshiba baada ya kuzungumza na mastaa wa fani mbalimbali Bongo na
kueleza sababu za wao kubadili usiku kuwa mchana.
SHOO / BATA
Hemed Suleiman
(filamu/muziki)
Kutokana na namna
kazi ya muziki ilivyo, wasanii wa muziki hulazimika kukesha usiku kucha
wakipiga shoo katika kumbi mbalimbali na kurudi majumbani alfajiri na hivyo
kupumzika mchana.
Hilo linawekwa
sawa na msanii wa filamu ambaye pia ni mwanamuziki, Hemed Suleiman ‘PhD’
aliyesema kwamba, muda wake wa kulala huwa kati ya 10 – 11 alfajiri.
“Kazi inasababisha
iwe hivyo. Kuna wakati labda nina scene za kucheza usiku, kama ni nyingi basi
nalazimika kulala mchana mzima ili usiku niweze kwenda kufanya kazi nzuri.
“Usisahau kuwa
mimi pia ni mwanamuziki, wakati mwingine huwa natakiwa kwenye shoo, kama
unavyojua tena shoo nyingi ni za usiku kuliko mchana. Hiyo ndiyo husababisha
nishindwe kufuata utaratibu wa kawaida wa maisha ya binadamu unavyopaswa,”
anasema Hemed.
Rubby (mwanamuziki)
Kwa upande wake
Hellen George ‘Rubby’ amesema mastaa wengi hufanya shughuli zao usiku, huku
wakati mwingine wakikutana kwenye kumbi za burudani.
“Kazi nyingi huwa
tunafanya usiku, kama sina kazi basi nitakwenda kwenye kumbi za burudani.
Unajua huko kunakupa msanii mwanga katika kazi zako. Ukitazama shoo ya
mwenzako, lazima kuna vitu utajifunza.
“Mimi huwa nalala
kati ya saa sita au saba kama sina mtoko, muda ambao huwa nautumia kuandika
mashairi yangu, lakini kama nimetoka huwa nalala kati ya saa 10 – 11 alfajiri.
Muda wa kuamka sina, nitatoka kitandani pale nitakapoona mwili wangu umepumzika
vya kutosha,” anasema Rubby.
UTULIVU
Snura Mushi
(filamu/muziki)
Sababu nyingine
inayowafanya mastaa kubadilisha usiku kuwa mchana, inaelezwa kuwa ni kutafuta
utulivu wa akili wakati wa kutunga kazi zao.
Hoja hii inaungwa
mkono na msanii wa filamu na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ambaye anasema:
“Huwa natunga nyimbo zangu usiku. Ni muda ambao umetulia na kichwa kinaweza
kufanya kazi na kufikiri vizuri. Usiku ni mzuri kwa kutunga maana hata vurugu
za watoto nyumbani zinakuwa zimeshapungua kabisa.”
Snura anasema mara
nyingi muda wa kulala huwa kati ya saa 9 – 11 alfajiri kulingana na namna
atakavyokuwa amechoka, huku akiamka kati ya saa 6 – 7 mchana.
Hussein Tuwa
(mtunzi wa riwaya)
Mtunzi mahiri wa
riwaya nchini, Hussein Tuwa naye alipohojiwa na Juma3tata kuhusiana na ishu
hiyo alikiri, akieleza sababu ni kutafuta utulivu wa kuumba maneno kwa utulivu.
“Riwaya ndiyo mama
wa sanaa zote unazoziona. Kwa mfano filamu au muziki. Msanii wa filamu hawezi
kuingia location kama hana mswada ambao utakuwa umeandikwa na mwandishi.
Kadhalika hata msanii wa muziki, hawezi kuingia studio kurekodi kama hana
mashairi.
“Kutokana na hayo
dada yangu (mwandishi), lazima kichwa kitulie sana wakati wa kuandika riwaya.
Mara nyingi huwa napenda kutulia usiku nikitunga kazi yangu. Lakini hata kama
sitakuwa na kazi ya kuandika, kama mwanafasihi lazima nisome vitabu vingi na
kutazama filamu mbalimbali ili kukuza ufahamu wangu.
“Nakumbuka wakati
naandika kitabu changu cha Mkimbizi, asimilia 70 ya muda nilioandika ilikuwa
usiku. Utulivu wa usiku ndiyo unaowafanya watunzi wengi wapende kutulia usiku
na kupumzika mchana,” anasema Tuwa ambaye ni Rais wa Umoja wa Waandishi wa
Riwaya Wenye Dira Tanzania (Uwaridi).
Tuwa anaongeza:
“Nashukuru kwamba kwa utulivu ninaoupata usiku, basi huwa naandika kazi nzuri
ambazo zimeniongezea mashabiki wengi ndani na nje ya nchi, maana huwa naandika
pia vitabu kwa lugha ya Kiingereza.
“Kwa kawaida huwa
nalala kati ya saa 6 – 7 usiku kama sina kazi ya kuandika, lakini kama siku
hiyo naandika naweza nikalala hata saa 11 alfajiri.”
Yusuph Mlela
(msanii wa filamu)
Staa wa filamu za
Kibongo, Yusuph Mlela anasema yeye huamua kulala mchana na kufanya kazi zake
usiku kwa sababu ya kutafuta utulivu kama walivyotangulia kueleza Snura na
Tuwa.
“Kwa kawaida huwa
nalala saa 11 alfajiri na kama ikitokea nikawahi sana basi ni saa 9, kuamka ni
kati ya saa 8 – 9 mchana ili kujiepusha na uzee wa wa usinginzi. Napenda
kufanya shughuli zangu usiku, mchana inabidi tuwaachie watu walioajiriwa, usiku
ni muda wa sisi tuliojiajiri,” anasema Mlela na kuongeza:
“Lakini pia kuna wakati
mtu unataka kwenda kula bata, huwezi kufanya kazi muda wote, kama staa lazima
upate muda wa kutoka ili kupanua mawazo na kukutana na watu tofauti.”
IRENE UWOYA
(msanii wa filamu)
Uwoya anasema yeye
huchelewa kulala kwa sababu ya mizunguko yake (mitoko) au kazi zake za kisanii
zinazofanyika usiku wakati mwingine.
“Sina ratiba
maalum, lakini kwa kawaida huwa nalala kati ya saa 10 – 11 alfajiri na kuamka
kati ya saa 7 – 9 mchana. Sasa itategemea kama labda nilikuwa location kwa
ajili ya kurekodi filamu au nimetoka na mambo mengine lakini usiku ni muda
wangu wa kufanya mambo yangu na mchana ni muda wa kulala,” anasema Uwoya.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Hemedy
PHD atashare siku yake ya kuzaliwa na mwanae.
Muimbaji
na muigizaji huyo wa filamu, Jumanne hii, October 30 amesherehekea siku yake ya
kuzaliwa na pia kuzaliwa kwa mwanae.
Akishare
picha hiyo juu, Hemedy aliandika kwenye Instagram: YOU GOD FOR THE BLESSINGS!!
HAPPIEST&LUCKIEST MAN ALIVE!! HAPPY TO BE UR FATHER! HAPPY TO SHARE THE
SAME BIRTHDAY WITH MY OWN BLOOD!DAMN WE MADE HISTORY.”
“WELCOME
TO THE WORLD BABY, THE NEW VERSION OF ME! MY LEGACY! 30TH AUGUST#ProudDad
#FatherOftheYear #VIRGOCHOSEN. HAPPY BIRTHDAY TO US,” aliongeza.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Nyota wa muziki wa Pop nchini Marekani, raia wa Canada,
Aubrey Drake, amesema alianza kumpenda mpenzi wa zamani wa Chris Brown, Rihanna
tangu alipokuwa na miaka 22.
Drake ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 29, amedai kuwa
alianza kuwa karibu na Rihanna miaka ya nyuma, lakini alishindwa kuonyesha wazi
ila kwa sasa kila mmoja anajua kuwa wawili hao wapo karibu.
“Nilianza kuvutiwa na Rihanna nikiwa na miaka 22,
lakini sikuonyesha chochote kwake, lakini kwa sasa nimeweza kufanikiwa kuwa
naye.
“Hakuna chochote kinachoendelea kati yetu zaidi ya
urafiki wa karibu kutokana na kazi zetu za muziki na si vinginevyo,” alieleza
Drake.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Chris
Brown amekamatwa na polisi wa LAPD kwa madai kuwa amemtishia mtu kwa silaha
nzito.
Baylee
Curran alimshutumu Brown kwa kumtishia na bunduki yake huko Tarzana, Calif.
Mrembo huyo aliyekuwa akijirusha na Brown kabla ya hapo, anadai kuwa ugomvi
ulizuka baada ya kuonesha kutamani midani zake za madini.
Muimbaji
huyo alidai kumfukuza msichana huyo na kumtishia na bunduki.
Maofisa
wa polisi waliwasili kwenye eneo la tukio saa tisa alfajiri Jumanne hii baada
ya simu ya 911 kupigwa na mwanamke aliyehitaji msaada. Curran alipeleka
mashtaka polisi na kukatolewa hati ya kufanywa msako.
Wakati
wa uchunguzi, Brown anadaiwa kutupa begi lake dogo nje ya dirisa ambamo
kulikuwa na bunduki mbili na madawa, kwa mujibu wa mtandao wa TMZ.
Baada
ya kulitupa, Breezy anadaiwa kupiga yowe ‘come and get me.’
Kwa
sasa amechukuliwa kwenye kitengo cha ‘Robbery Homicide’ kwenye LAPD.
Awali,
Brown alitumia Instagram kukanusha madai hayo.
“I’m
sleep half the damn night. I just wake up and all these motherfuckin’
helicopter choppers is around, police out there at the gate. Come on, my ni**a.
What the fuck else y’all want from me, bro? I stay out of the way, take care of
my daughter, do work. I don’t even fuck ugly bitches, triflin’ bitches.
Whatever the fuck it is, I’m not on that, bro…I’m innocent. Fuck everybody,”
anasema kwenye moja ya video hizo.
Brown
alikamilisha probation yake ya miaka mitano, mwaka jana ya tukio la
kumshambulia Rihanna. Hii inaweza kuwa kesi itakayomsumbua kwa mara nyingine
tena.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>