Video Information
Mkurugenzi wa mafunzo ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaj Arusha(AJTC) Aliyevaa koti jeupe akiwa na baadhi ya waalimu wa chuo hicho akisikiliza mada. |
Jumla ya wanachuo 227 wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wanatarajiwa kushiriki katika mafunzo ya ujasiriamali na mbinu za ukuzaji wa biashara, yatakayotolewa na wakufunzi wa chuo hicho
.
Akizungumza na blog hii mratibu wa mafunzo hayo Bwana Andrea Ngobole amesema kuwa: mafunzo hayo yatakuwa ya siku mbili kuanzia tarehe 19-20/09/2013na yanalenga kuwapa wanachuo hao juu ya mbinu na maarifa kuwa wajasiriamali na wafanyaiashara wenye mafanikio na kuwa chachu ya maendeleo kwa familia, jamii na taifa kwa ujumla
Amesema kuwa kitengo cha ujasiriamali chuoni hapo kimekuwa kikiandaa semina za ujasiriamali kwa wanachuo hao kila mwaka na kwa mwaka huu kinatarajia kuwasilisha mada 7 kutoka kwa watoa mada wanne ambao pia ni wakufunzi wa chuo hicho.
Semina hii itajumuisha mada kama Business Ventures, Business Networking na Business Family zitakazo wasilishwa na Neema Mwaipela pia kutakuwa na mada ya kutathimini biashara na misingi 10 ya ujasiriamali itakayowasilishwa na Ngobole pia Cash Flow Quadrant itakayowasilishwa na Adson Kagiye. Alisema Bw. Ngobole.
Ngobole amesema semina hiyo itatanguliwa na mada ya ufunguzi wa semina hiyo itakayowasilishwa na mgeni rasmi Bwana Joseph Kagiye Mayagila ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa mafunzo wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha ( AJTC )
Ameyataja madarasa yanayotarajiwa kushiriki katika semina hiyo kuwa niMKOMANZI, TANGANYIKA, SERENGETI, UDZUNGWA, RUWENZORI, KILIMANJARO, MANYARA, NYASA, KITENGO CHA ELIMU NA KOMPYUTA. na madarasa yaliyopo likizo kama SELOUS, NATRON RUAHA yataandaliwa semina mara watakaporejea kutoka likizo mnamo october au november kulingana na ratiba itakayotolewa na idara ya taaluma chuoni hapo