Video Information
Chelsea wameambiwa
wanaweza kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre
Emerick-Aubameyang, 28, kwa pauni milioni 60 baada ya Tianjin Quanjian
ya China kusema haitaki tena kumsajili mchezaji huyo. (Daily Mail)
Borussia
Dortmund huenda wakaamua kumfuatilia mshambuliaji wa Arsenal Olivier
Giroud, 30, ambaye pia anasakwa na Everton, West Ham, Marseille na AC
Milan. (Daily Mirror)Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26, amempigia simu meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane na kumuambia hana mpango wa kuondoka Chelsea msimu huu. (Diario Gol)
Chelsea wamefikia makubaliano na Monaco ya kumsajili kiungo Tiemoue Bakayoko, 22, kwa pauni milioni 40 kwa mkataba wa miaka mitano. (RMC)
Meneja wa Chelsea anajiandaa kumuuza kiungo Nemanja Matic, 28, kwa pauni milioni 40. Matic amekuwa akifanya mazoezi peke yake na anataka kuungana na Jose Mourinho Old Trafford. (Daily Telegraph)
Barcelona wanataka kumsajili beki wa Chelsea Cesar Azpilicueta baada ya kushindwa kumpata Hector Bellerin wa Arsenal. (Marca)
Chelsea watawazidi kete Juventus katika kumsajili beki wa kulia wa Real Madrid Danilo, 25, kwa pauni milioni 28. (Daily Mirror)
Mchezaji wa zamani wa Liverpool Danny Murphy amesema klabu hiyo inakaribia kukamilisha usajili wa Virgil van Dijk, 26, kutoka Southampton. (Sports360)
Arsenal wanataka kumsajili kinda wa West Ham Domingos Quina, 17. (Sky Sports)
Roma wanataka kumsajili winga wa Leicester City Riyad Mahrez, 26. (Sky Italia)
Tottenham wamesema hawatoburuzwa na Manchester United na Manchester City kuhusu usajili wa Eric Dier na Kyle Walker, huku wakikaribia kumsajili beki Juan Foyth, 19, kutoka Estudiantes kwa pauni milioni 9. (Daily Telegraph)
Manchester United wana matumaini ya kukamilisha usajili wa winga wa Inter Milan Ivan Persic, 28, wiki ijayo. (Daily Star)
Manchester United sasa wataelekeza nguvu zao kumsajili kiungo wa Roma Radja Nainggolan, 29, kwa kutoa pauni milioni 40 baada ya Tottenham kukataa dau lolote kuhusu Eric Dier. (Daily Mail)