Video Information
Msanii wa muziki kutoka nchini Uingereza Adele, amelazimika kukatisha
tamasha lake la 123-date world tour kwa kile kinachodaiwa kupata
madhara katika koo lake(vocal cords).Muimbaji huyo mwenye mashabiki lukuki amelazimika kukatisha show zake mbili zijazo baada ya show yake ya Juni 29 aliyofanya uwanja wa Wembley nchini humo. Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram jana aliamua kuwaandikia mashabiki zake waliokuwa wakiisubiria tamasha hilo kuwa atashindwa kuendelea na tamasha kutokana na maradhi aliyonayo.
Mwaka 2011 Adele aliwahi kufanyiwa upasua wa ‘polyp’.