Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

Nikki wa Pili, Waziri Njenje wachambua muziki wa zamani na Bongo Fleva

Views:
Video Information
Msanii mkongwe kutoka  Kilimanjaro Band (Njenje), Waziri Ally Njenje ameketi sehemu moja na msanii wa Bongo Fleva kutoa kundi la Weusi, Nikki wa Pili na kwa pamoja wameweza kuchambua muziki wa zamani na wa sasa (Bongo Fleva).
Nikki wa Pili na Waziri Ally Njenje
Wakizungumza katika kipindi cha Amka na BBC cha Idhaa ya Kiswahili ya BBC, wameeleza sababu ya muziki zamani kudumu kuliko wa sasa, namna wasanii wa pande zote mbili wanavyoweza kushirikiana na jinsi tungo zao zinavyoweza kugusa maisha ya sasa.
Nikki wa Pilii ameeleza sababu ya muziki wa sasa kutodumu kipindi kirefu inatokana na msukumo mkubwa wa muziki wa sasa kujikita katika  soko au kupata fedha, kwa hiyo wasanii wanaangalia kile ambacho kinaweza kuwapatia fedha kwa muda huu.
“Ukiangalia muziki wa Njenje tunaweza kusema asilimia mia ulikuwa ni msukumo wa muziki, kwa hiyo ulikuwa unazingatia vitu vingi lakini sasa hivi ni muziki wa soko na ili soko liende na tasnia iendelee ni lazima bidhaa zitoke na kuingia,” amesema Nikki na kuongeza.
“Kwa hiyo ni muziki wenye mapokeo ya kisoko lakini tasnia yenyewe imekaa kisoko haitoi nafasi kwa muziki kukaa muda mrefu kwa sababu kisoko sio nzuri na haina faida,” ameeleza Nikki.
Kuhusu hilo Waziri Njenje amesema, “kwanza tulikuwa tunathamini sana asilia zetu, kwa mfano ukiangalia Njenje tunachuka sana nyimbo za makabila haya na kuweza kuingiza hisia zetu, na tunapokuwa tunacheza katika mashughuli zetu unakuta makabaila tofauti wanacheza nyimbo zile zile, kufanya hivyo ni moja ya sababu muziki wetu kudumu kwa muda mrefu”.
Kwa upande wake Nikki kuhusu wasanii wa sasa na wa zamani kushirikiana (collabo), amesema wasanii wa kipindi hiki wana-sound nyingi za kuchukua kutoka kwa muziki uliotangulia na kufanya hivyo ni namna ya kutunza na kuenzi zile classic songs.
“Sisi tumeshafanya nyingi, kuna kipindi ambacho tulikusanya vijana wa Tanga tukafanya nao collabo moja nzuri tu, lakini pia tumefanya na Mwana FA na juzi hapa tumefanya na Kassim Mganga,” amesema Waziri Njenje.
Katika hatua nyingine Nikki ameeleza jinsi muziki wao unavyoweza kuenzi utamaduni uliopo, “mchanganyiko wa muziki na mataifa mengine upo sema sisi katika muziki wa rap, ingawa rap ni ya Marekani lakini tunajaribu kueleza historia za maisha yetu ya uswahilini tunapoishi, kwa hiyo sisi tumeiga huo mtindo wa kuflow lakini maudhui tunawakilisha mitaa ambayo tunatoka,” amesema Nikki wa Pili.
By Peter Akaro Wa Bongo5
Similar Videos