Video Information
Msanii wa Gospel, Angel Bernard na hitmaker wa wimbo ‘I Need You To
Reign’, ameelezea undani wa wimbo wake ‘Ni Salama’ ambao ulitumika
kuwafariji wafiwa wa ajali ya Lucky Vicent iliyoua wanafunzi zaidi ya 30
mkoani Arusha.Akizungumza na Kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, muimbaji huyo amesema alitunga wimbo huo kutokana na mambo kadhaa aliyokuwa anapitia katika ndoa yake.
“Ni salama ni wimbo wa vitabuni wakristo huwa wanaimba kwa namna nyingine lakini kwangu mimi kulikuwa kuna kipindi tunapitia na mume wangu mapema sana baada ya kuoana kuna mambo mengi tulikuwa tunakutana nayo na huu wimbo ulikuwa ni matokeo ya kujiambia sisi ni salama pamoja na mambo yote,” amesema na kuongeza.
“Mume wangu alipendekeza idea ya huu wimbo mimi nikaandika na ukawa hivi, makanisani hawaimbi hivi kwa hivyo vitu vingi tulivibadilisha ili viendane na sisi na kipindi ambacho tulikuwa tunapitia,” amesistiza Angel.
Pia Angel ameongeza kuwa amekuwa akifanya project mbali mbali na THT kwa kipindi kirefu sasa ambacho ni zaidi ya miaka minne ila mara nyingi amekuwa akiitwa (THT) kulingana na project husika kutokana yeye amejikita zaidi katika gospel na masuala ya kitaifa.