Video Information
Mmoja kati ya wasanii wanaounda Kundi la Yamoto Band, Aslay, ambaye
hivi sasa ameanza kufanya kazi peke yake nje ya kundi hilo, amefunguka
kwa kudai kuwa kuna vitu vimewakwamisha na kushindwa kwenda mbele kama
kundi.
Yamoto Band
“Mimi nafikiri kwamba mipango yetu tu wenyewe, kipindi kile tunatoa ile video ‘ Madoido’ kulikuwa na show nyingi zinaongozana ambazo zilituzuia kwenda kutengeneza video nyingine lakini si unajua tulikuwa tunajenga pia kwa hiyo kifupi ni kama tulijisahau na kuteleza kusema ukweli,” alisema Aslay.
Aliongeza, “Tukarudi tena tukafanya ‘Suu’ ambayo tuliifanya Zanzibar na tukawa na pesa kabisa ambayo ingetuwezesha kutengeneza video nyingine Afrika Kusini lakini hapo katikati tulifanya vitu fulani mchanganyiko ambavyo siwezi kuvisema vikaturudisha tena nyuma” alisema Aslay
Mbali na Aslay msanii mwingine kutoka kundi hilo Beka Flavour naye ametoka na wimbo wa peke yake akiwa chini ya menejimenti nyingine.