Video Information
Msanii wa muziki aliyewahi kufanya vizuri na wimbo ‘My’, Ally Nipishe
amefunguka kuzungumzia kitu ambacho kinafanya nyimbo zake nyingi za
hivi karibuni zishindwe kufanya vizuri.
Ally Nipishe
Ally amedai nyimbo zake nyingi zimeshindwa kufanya vizuri kutokana na kukosa usimamizi.
“Unajua muziki umebadilika sana, unahitaji usimamizi mkubwa sana tofauti zamani,” alisema Ally Nipishe.”Kusema kweli ngoma zangu za zamani kama ‘My’ ilipata usimamizi mzuri sana tofauti na nyimbo zangu za hivi karibuni ingawa zinasimawiwa lakini bado hatujafika sehemu ambayo tunahitaji kufika,”
Muimbaji huyo ambaye yupo chini ya Papa Misifa, amedai kwa sasa anajipanga zaidi ya management yake ili kuhakikisha anarudi kwenye chati kama zamani.