Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya kutoka moshi mkoani Kilimanjaro Yayah Prince amesema kisa cha kubadilisha A.k.a kutoka Man sing hadi yayah Prince ni kutokana na jina la man sing kuwa gumu.
Akizungumza na Fleva no limit ya Redio Kibo FM Leo ijumaa tarehe 20 Jan 2017 na Deo Kessy the heavyweight presenter amesema alifanya uchunguzi wa kina na kuona jina hilo ni gumu hususani katika mitandao ya kijamii
"Hilo jina lilikuwa gumu sana kwenye mitandao ya kijamii ulikuwa ukinitafuta unakutana na wenye Sing nyingi so wadau wakashindwa kunipata"amesema Yayah Prince
Ameongeza Jina la Yayah Prince lilishinikizwa na Producer Laizer wa WcB alipomwambia anabadilisha
"Nilimwambia Laizer hili jina gumu sana akasema ni kweli tafuta jingine simple ndipo nikafikiria jina la babu yangu Yahaya nikachekecha akili nikapata Yayah Prince"
Pia amesema ngoma yake ya Lavo ni ngoma nzuri kwani ameifanyia nyumbani Kilimanjaro Audio na Video.
Kuhusu WCB amesema kuna ngoma kafanya pale na tayari kafanya final soon ataitoa.
Amehitimisha kwa kuwataka wadau wa mziki mzuri kutoka Kilimanjaro kuendekea kumsaport kwa nguvu kwani hatowaangusha kamwe.