Video Information
Baadhi ya wakazi wa Mombasa nchini Kenya wamevutiwa na sera na utendaji kazi wa Rais Dkt John Magufuli na kuwataka viongozi wengine barani Afrika kuiga kutoka kwake. Wameyasema hayo mjini Mombasa kwa kutoa ushauri kwa viongozi wa nchi za Afrika Mashariki kuiga mfano wa Dkt Magufuli.

Hili ni jiji la Mombasa kutoka juu
Wakazi hao walipohojiwa kuhusu utendaji kazi wa Rais Magufuli kila mmoja aliweza kutoa maneno yake kwa mitazamo tofauti tofauti.
“Eh Magufuli alivyochaguliwa tulifurahi sana kwasababu ana muelekeo mzuri wa wa Afrika wenzetu kwasababu vile alichaguliwa pia hapo Kenya tulisherehekea sana na ile siku yake ya kwanza ya kuingia katika kile kiti tulimuona akifagia kule Dar es Salaam na hilo lilitupa muelekeo wa Rais kufagia na wananchi wa kawaida”, alisema moja ya mkazi wa Mombasa aliekutwa katika fukwe hizo.
Na huku mwingine akisema kuwa yeye anamuona Dkt Magufuli ni kiongozi bora, mzuri, na pia alisema kuwa ni kiongozi mwema.
Aidha Wakazi hao waliwataka viongozi na Marais nchi za Afrika Mashariki kushirikiana pamoja kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wao.
“Afrika Mashariki mi naomba washikane pamoja ndiyo wananchi wapate faida na wafanye biashara wote pamoja mambo itakuwa sawa sawa,” alisema mfanyabiashara mmoja katika eneo hilo.
Ikumbukwe kuwa Mombasa ni mji uliopo pwani ya bahari ya Hindi ukiwa ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Kenya na pia ni kitovu cha biashara ya utalii wa pwani ya bahari ya taifa hilo.