Video Information
Mamla ka ya hali ya hewa nchini TMA
imewatahadharisha Wananchi pamoja na Taasisi mbalimbali ikiwemo za Uokoaji,kujiandaa
juu ya namna ya kukabiriana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za
masika ambazo tayari zimeanza kunyesha hapa nchini.
Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Dkt.Agness Kijazi ametoa
tahadhari hiyo juzi Jijini Mwanza,wakati akitoa taarifa ya mwelekeo wa Mvua za
Masika kwa Kipindi cha kuanzia mwezi Machi hadi mwezi Mei Mwaka huu.
Dkt.Kijazi amesema kuwa mvua za Masika zinatarajiwa
kuanza katika wiki ya kwanza nay a pili ya mwezi machi mwaka huu, katika maeneo
ya Ukanda wa Ziwa na kusambaa katika maeneo mengine yanayopata misimu miwili ya
mvua kwa mwaka.
Amesema Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi
juu ya wastani katika maeneo mengi nchini, na kwamba zinaweza kusababisha
athari mbalimbali ikiwemo mafuriko hivyo ni vema wananchi pamoja na mamlaka za
uokozi zikajiandaa kikamilifu ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.www,sayariblog.blogspot.com