Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

Bomu la laptop lalipuka Somalia

Views:
Video Information



Image copyrightThinkstock
Image captionBomu ya Laptop yalipuka Somalia
Watu 6 wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea katika uwanja wa ndege ulioko mjini Beledweyne nchini Somalia.
2 kati ya wale waliojeruhiwa ni maafisa wa polisi huku wengine wakiwa raia.
Bomu hilo linaaminika kuwa lilikuwa limetegwa ndani ya kipakatilishi (laptop).
Mtu aliyekuwa ameibeba bomu hilo alikuwa anajaribu kuingia katika eneo salama katika eneo la upekuzi la Beledweyne takriban kilomita 325km nje ya Mogadishu.
Image copyrightDarren Howe
Image captionMwezi uliopita,kundi la kiislamu la Al- Shaabab lilidai kutekeleza shambulizi lililosababisha shimo kutokea katika ndege moja ya abiria.
Mwezi uliopita,kundi la kiislamu la Al-Shaabab lilidai kutekeleza shambulizi lililosababisha shimo kutokea katika ndege moja ya abiria.
Shambulizi hilo lilitekelezwa na bomu lililotegwa ndani ya kipakatilishi (laptop).
''Afisa wa ulinzi katika eneo hilo Luteni Kanali Ali Dhuh Abdi amesema kuwa bomu hilo lililipuka kisha maafisa wa usalama wakaharibu mabomu mengine 2 yaliyokuwa yametegwa ndani ya kipiga chapa (printer)
Similar Videos