Video Information

Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Mijimwema mjini Njombe, mkoani Njombe, Monica Kiongosi
wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi baada ya kikao cha kufungia
shule, ambapo pamoja na mambo mengine wazazi walipewa ripoti za watoto
wao. Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 818 na walimu 20 amabpo mwalimu
wakiume ni mmoja tu. Changamoto nyingine ni upungufu wa madawati,
matundu ya vyoo yaliopo ni matundu 12, nyumba za walimu pamoja na
madarasa.

Wanafunzi
wa shule ya Msingi Mjimwema mjini Njombe, mkoani Njombe wakiosha sahani
kisimani kabla ya kwenda kupiga foleni ya kupata chakula cha mchana
ambapo mara nyingi ni kande. Shule hiyo inatumia maji ya kisima baada ya
mfumo wa maji ya bomba kuchakaa.

Msimamizi
wa Zahanati ya Mjimwema, Debora Kyejo (kushoto) akionyesha baadhi ya
dawa zilizopo katika chumba cha dawa wakishirikiana na Melisiana Mhagama
walipotembelewa na mwandishi wa gazeti la kwanzajamii hivi karibuni.
Zahanati hiyo ilijengwa kwa nguvu za wananchi na ina changamoto
mbalimbali kama vile upungufu wa watumishi waliopo ni watumishi wa tatu,
haina daktari, haina vitanda vya kufanyia uchunguzi (examination beds)
na vitanda vya kujifungulia vilivyopo ni vitanda viwili na umeme.

Mafundi
wakiendelea kuezeka mabati kwenye darasa la awali ambalo limeanza ujenzi
wake kwa muda mrefu bila kukamilika. Shule ya Msingi Mjimwema haina
darasa la awali inatumia chumba kimoja kwa ajili ya wanafunzi 139 ambapo
hata hivyo wanalazimika kusoma kwa zamu. Wanafunzi hao wanakalia
madawati ya kawaida badala ya mawadati kwa jili yao maalum.

Wanafunzi wakiwa katika foleni ya kupata chakula cha mchana.

Mpishi akiendelea kupita chakula cha wanafunzi ambapo mara nyingi ni kande.