Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

Jinsi ya kujipulizia pafyumu kichwani

Views:
Video Information





Kwa wanawake wengi ni jambo la kawaida kupulizia manukato mbalimbali katika sehemu za miili yao ikiwamo kichwani. Manukato hayo hujumuisha udi, pafyumu hata mafuta mazuri.

Iwe ni kwa ajili ya kuongeza manukato mwilini ama kuboresha mwonekano, matumizi ya pafyumu katika nywele yamekuwa yakisababisha athari tofauti katika nywele ikiwamo kudhoofika hatimaye kukatika. Mara nyingi jambo hili husababishwa na uwepo wa alcohol katika pafyumu.

Ikiwa mtu atajipulizia bila kuwa na tahadhari, anaweza kupata matatizo hayo na mengine kichwani kwake.

Kwa kutambua hilo wataalamu wa mambo ya afya na urembo wamekuja na dondoo mbalimbali za jinsi ya kujipulizia pafyumu kichwani ili kusaidia kukuepusha na matatizo hayo niliyotaja hapo juu.

Ikiwa dondoo hizi zitafuatwa kwa makini, mtumiaji anaweza kutumia pafyumu yeyote anayopendelea bila kusababisha madhara kwa nywele zake.

Njia ya kwanza ni kujipulizia pafyumu nyuma ya masikio, shingoni na maeneo mengine yanayozunguka nywele zako.

Mbali na njia hiyo, kwa kuwa baadhi ya kemikali zilizoko kwenye pafyumu zina uwezo mkubwa wa kuathiri nywele zako, unachotakiwa ni kuepuka na kuzuia zisiguse nywele zako.

Kwa mantiki hiyo, unaweza kupulizia pafyumu kwenye kitana ama shanuo unalochania nywele zako na baada ya kuhakikisha kuwa pafyumu hiyo imekauka chana nywlele zako. Kwa kufanya hivyo, ile harufu nzuri itabaki kwenye nywele zako bila kuwa na kemikali nyingine.

Wakati mwingine inawezekana kuwa unahitaji nywele zako zinukie, lakini huitaji kuzichana kwa muda huo. Ikiwa hilo litatokea, unashauriwa kupulizia pafyumu katika viganja vya mikono yako na baada ya muda pangusa mikono yako katika nywele.
Similar Videos