Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

Bilal akemea uharibifu mazingira

Views:
Video Information




Na Ellah Daniel.
Mwanza. Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal ameonya watu kuacha kujihusisha na uvuvi haramu, uchomaji moto na ukataji miti ovyo ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.


Akihutubia kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani hapa jana, Dk Bilal alisema zamani dunia ilikuwa na viumbe hai vingi, lakini vimepotea kutokana na mabadiliko ya tabianchi.


“Watanzania tushirikiane na Serikali kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ikiwamo kutojihusisha na uvuvi haramu, kuchoma moto na ukataji miti ovyo ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,”alisema Dk Bilal.


Akitangaza tuzo za washindi wa usafi wa mazingira, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid alisema wizara imeendelea kuboresha usafi wa mazingira ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko.


Dk Rashid alisema mazingira machafu yanaathiri watoto walio chini ya miaka mitano, jambo ambalo ni hatari kwa afaya.


Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo alisema wataendela kutunza na kuhifadhi mazingira baada ya kushinda Tuzo ya Jiji Bora kwa Usafi wa Mazingira.


Wakati huohuo, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Kitengo cha Anwai za Jamii, Salome Kaserma amewataka wananchi Mkoa wa Mwanza kuiga Mkoa wa Kilimanjaro kwa utunzaji mzuri wa mazingira.


Akizungumza kwenye upandaji miti na kusafisha mazingira eneo la Igoma, Kaserma alisema wananchi wanatakiwa kutunza mazingira ambayo yana faida kubwa kwa maisha ya binadamu.


“Kila Mtanzania anatakiwa kuhakikisha anaishi mazingira salama, ili kuepukana na maradhi,” alisema.


Naye Ofisa Utumishi Uhamiaji Mwanza, Andrew Mwangolombe alisema kutunza mazingira ni jukumu la watu wote ili kuepukana na maradhi au njaa.


Nao wafanyakazi wa Kituo cha Afya AAR Mwanza, wamewaasa wananchi kudumisha usafi maeneo yao ili kuepuka magonjwa ya milipuko.


Muuguzi Mkuu wa kituo hicho, Zuhura Tamla alisema jamii haina budi kuzingatia usafi kwenye mazingira yanayowazunguka.
Similar Videos