Video Information
Raia wa Ukraine kila uchao wanazidi kuwasilisha maombi kwa ajili ya kuishi huko Russia. Nikolai Gavrichkov, Msemaji wa Idara ya Uhamiaji ya Shirikisho la Russia ameeleza kuwa kiwango cha maombi yanayotolewa na raia wa Ukraine wanaotaka kubatiwa kibali cha kuishi huko Russia yameongezeka mara saba.
Gavrichkov ameongeza kuwa tangu mwanzoni mwaka huu wa 2014, raia wa Ukraine zaidi ya elfu 20 wameomba kibali cha kuishi huko Russia huku wengine elfu 14 wameomba kupewa kibali cha kufanya kazi huko Russia.
Viongozi wa Russia wamesema kuwa maombi mengi yaliyowafikia ni kutoka maeneo ya kusini mwa Ukraine. Matukio ya hivi karibuni huko Ukraine yametoa msukumo kwa raia wa nchi hiyo kutaka kuhamia huko nchini Russia.