Video Information
Kundi la wanamgambo waliovamia
bandari za Libya zinazosafirisha
mafuta, limeiambia BBC kwamba
limeanza kusafirisha mafuta na
shehena ya kwanza ilipakiwa
kwenye meli yenye bendera ya
Korea Kaskazini.
Waziri mdogo wa mafuta
amethibitisha kuwa meli hiyo
imefunga gati katika bandari ya Sidr
ambayo inadhibitiwa na kundi
linalotaka kujitenga.
Serikali ya Libya inashindwa kuanza
tena kusafirisha mafuta hadi nchi
za nje kwa sababu ya migomo katika
bandari na visima vya mafuta
kutekwa na wanamgambo.
Serikali inahitaji pato linalotokana
na mafuta ili kuendesha uchumi wa
nchi.