Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

VIGOGO WATOA DOZI LIGI ZA ULAYA

Views:
Video Information
ronaldo_de10e.jpg
London, England. Wakati vinara watatu wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga wakishinda, hali haikuwa hivyo England baada ya vinara kushindwa kupata ushindi Jumamosi.
Chelsea waliendelea kuongoza ligi pamoja na kufungwa 1-0 na vibonde Crystal Palace baada ya mahasimu wake katika mbio za ubingwa Arsenal na Manchester City kutoka sare 1-1, kabla ya mchezo wa jana usiku kati ya Liverpool na Tottenham.
Washambuliaji nyota katika La Liga wote walifunga magoli huku Diego Costa akiiongoza Atletico Madrid kubaki kileleni, akifuatiwa na Lionel Messi wa Barcelona, na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.
HISPANIA
Atletico wameendelea kusaka ubingwa wao wa kwanza tangu 1996, baada ya Diego Costa kufuta bao la Iker Muniain na Koke "Jorge" Resurreccion akifunga bao la pili kwa vinara hao walipoichapa Athletic Bilbao 2-1.
Lionel Messi alifunga bao kwa mkwaju wa penalti na kuifanya Barcelona kuwa nyuma kwa pointi moja kwa Atletico waliposhinda 1-0 dhidi ya Espanyol.
Cristiano Ronaldo alifunga bao moja kabla ya Gareth Bale kufunga mawili wakati Real Madrid ilipoisambaratisha Rayo Vallecano 5-0, wakitoa hasira zao baada ya kufungwa katika michezo miwili mfululizo.
ITALIA
Mario Balotelli alifunga bao moja na Kaka aliongeza mawili wakati AC Milan ilipowachapa vibonde Chievo Verona 3-0 na kumpa kocha Clarence Seedorf ushindi wa kwanza tangu alipochukua jukumu hilo Januari.
Ushindi huo umewafanya Milan kulingana na Lazio katika nafasi ya nane, pointi sita nyuma ya Inter Milan katika kusaka nafasi ya tano ya kucheza Europa Ligi.
UFARANSA
Monaco imefungua njia kwa Paris Saint-Germain kuchukua ubingwa msimu huu, baada ya kufungwa 1-0 na Evian. PSG iliichapa Nice 1-0, Ijumaa na kuiacha Monaco kwa pointi 13 ikiwa imebakiza michezo saba.
Similar Videos