Wachagga ni kabila la watu wenye
asili ya Kibantu wanaoishi
kaskazini mwa Tanzania chini ya
mlima Kilimanjaro, mkoani
Kilimanjaro. Shughuli kubwa ya
Wachagga ni biashara na kilimo.
Wachagga ni kabila la tatu kwa
ukubwa nchini Tanzania. Takwimu
za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa
idadi ya Wachagga mkoani
Kilimanjaro ni 200,000.
Vikundi vya Wachagga
Wachagga wana historia ndefu ya
asili yao na maingiliano yao na
makabila mengine. Kabila la
kichagga ni mkusanyiko wa
makabila madogo madogo (ya
Kichagga) yaliyosambaa kijiografia
kuzunguka mlima Kilimanjaro
kuanzia Mashariki Tarakea, Rombo
hadi magharibi ya Kilimanjaro
Siha, Machame. Makabila ya
Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-
Marangu,Wa-Kilema, Wa-Old
Moshi, Wa-Kibosho, na Wa-
Machame. Makundi mengine
madogo ya wachagga ni Wakirua-
Vunjo, Wa-Uru, na Wa-Siha.
Lugha ya Kichagga
Lugha ya Kichagga, inabadilika
kuanzia unapotoka Tarakea mpaka
unapofika Siha magharibi mwa
Kilimanjaro. Kutokana na tofauti
hizo Kichagga kimegawanyika
katika Kirombo, Kimarangu, Ki-Old
Moshi,Kikibosho, Kimachame,
Kikirua na Kisiha. Lugha hizi
zinakaribia kufanana kulingana na
jinsi makabila hayo yalivyopakana.
Kwa mfano, Ki-Marangu kinafanana
na Kikirua. Vile vile Kisiha
kinafanana sana na Kimachame
ambacho pia kinafanana kidogo na
Kikibosho. Baadhi ya Wamachame
walihamia sehemu za Meru Arusha
na kuchanganyikana na Waarusha ,
lugha yao ikabadilika kidogo na
kuwa Ki-meru. Kwa sababu hii
Wameru wanasikilizana sana na
Wamachame ingawa lafudhi zao
zinatofautiana kidogo.
Historia ya elimu kati ya
Wachagga
Wachagga wanajulikana kwa uwezo
wao mkubwa wa kufanya biashara
na pia kilimo. Moshi ni maeneo ya
mwanzo ambayo Wamisionari wa
Kikristo walijenga makanisa na
shule. Sababu hii imefanya
Wachagga kuwa kabila lenye watu
wengi zaidi walio na elimu ya
kisasa na mkoa wa Kilimanjaro
unaongoza kwa idadi ya shule za
sekondari nchini Tanzania.
Kulingana na takwimu za elimu
mkoa wa Kilimanjaro una shule za
sekondari zaidi ya 320. Pia mkoa
una shule za msingi zipatazo 950.
Idadi hii ya shule ni kubwa zaidi
ya idadi ya shule katika mikoa
mingine Tanzania.
Shule nyingi za sekondari ziko
katika mkoa huu kwa sababu
zifuatazo: 1) Hali ya hewa na
vivutio vya kitalii katika mkoa huu
viliwavutia zaidi walowezi na
wakoloni na kuweka makazi yao
hapo. Hivyo wamishinari walijenga
shule za kwanza wakifuatiliwa na
serikali za wakoloni 2) Serikali ya
Tanzania ilirithi shule zilizojengwa
na wakoloni 3) Wachagga
waliobahatika kupata fedha binafsi
baadaye waliwekeza kwenye ujenzi
wa shule binafsi kama kitega-
uchumi. Wakati wakazi wa mikoa
mingine walisubiri serikali
iwajengee shule. 4) Ukichanganya
sababu 1,2 & 3 utagundua shule
katika mkoa Kilimanjaro vimezidi
sana idadi ya shule katika miko
mingine yote.
Ni vema pia kusema kwamba shule
hizi kuvutia wanafunzi kutoka
Tanzania nzima, haziwasomeshi
wachagga tu.
Kilimo na chakula
Wachagga hulima mazao ya
chakula kama vile mahindi ,
maharagwe,viazi, ndizi , ulezi na
mboga mbalimbali. Mazao ya
biashara kama vile kahawa, nyanya
na vitunguu .
Ndizi za Wachagga
Ingawa wachaga wa leo wanakula
vyakula mbali mbali kama vile
ugali , wali na viazi, chakula kikuu
cha Wachagga ni ndizi. Kuna ndizi
za aina mbalimbali na hutumika
kwa matumiza tofauti. Mfano ndizi
kisukari ni fupi na huachwa hadi
ziive na huliwa mbivu kama
tunda. Ndizi mshare kukatwa
zikiwa mbichi na kupikwa chakula
mbalimbali pamoja na nyama ya
ngombe, kondoo au mbuzi. Mara
nyingine hupikwa na maharage,
choroko,kunde au hata maziwa ya
mtindi. Vyakula vya ndizi huja kwa
ladha tofauti kama vile ndizi
nyama, mtori, machalari, kiburu na
kadhalika.
Aina nyingine ni ndizi-ngombe
ambazo huachwa ziive halafu
humenywa na kutumiwa
kutengenezea pombe maarufu
iitwayo mbege . Mbege
hutengenezwa kwa kutumia ndizi
mbivu, maji, na ulezi.
Aina nyingine ni ndizi-mzuzu. Hizi
zikikomaa huachwa zianze kuiva
kidogo halafu huchomwa na kuliwa
kama kitafunwa pamoja na chai au
pombe. Ukipita mitaa ya
Darisalamu utaona ndizi- mzuzu
zikichomwa sambamba na muhogo
au kuku-vumbi au kiti-moto.
Wachagga na muhogo
Inasemekana kuwa "mchagga
halisi, hali muhogo - akila muhogo
atakufa". Usemi huu umetokana na
historia ya mababu kuwa
wachagga waliopanda mihogo
Kilimanjaro enzi za kale walikufa
baada ya kuila. Historia hiyo
yaweza kuwa ya ukweli kwa sababu
aina nyingi za mihogo zinajenga
sumu ya sianidi ndani yao; watu
waliozoea kutumia mihogo huwa
na njia za kuondoa sumu kwa kwa
kuiloweka mihogo katika maji kwa
muda. Lakini kama Wachagga wale
wa zamani hasa wa Machame
walifanya jaribio bila kujua mbinu
ya kuondoa sumu ajali iliweza
kutokea. Cha kushangaza ni
kwamba huko huko Kilimanjaro,
majirani na watani wa wachagga
yaani Wapare walikuwa
wameshazoea mihogo na ilikuja
kuwa moja ya chakula chao kikuu.
Ulaji kiti-moto
Pamoja na kilimo cha mazao,
wachagga hupendelea sana kufuga
nguruwe. Tabia ya kula nyama ya
nguruwe ijulikanayo leo kwa jina
la "kiti moto" ni moja ya mambo
yaliyoenezwa na wachagga. Ulaji
wa "kiti moto" haukupendeza
baadhi ya wenyeji wa Pwani kama
Dar es Salaam ambapo wachagga
walihamia, kwani wakaaji wengi wa
Pwani ni Waislamu kwa hiyo
nguruwe kwao ni haramu. Wakazi
wa Dar es Salaam watokao
makabila mengine na wasiyo
waisalmu kwao kula nguruwe
ilikuwa "ruksa".
Majina ya Kichagga
Majina ya kiukoo ya Kichagga pia
huashiria wanatoka sehemu gani
ya Uchaga, japo si lazima kuwa
hivyo: mfano familia maarufu za
Kichagga nchini Tanzania ni kama
ukoo wa akina Mushi,Kimaro, Swai,
Massawe, Lema, Urassa, Nkya,
Ndosi, Meena hutoka Machame.
Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo,
Moshiro, Mselle, Kileo, Kimambo,
Tesha wanatoka Old Moshi na
Vunjo. Kavishe,Mariki, Tarimo,
Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda,
Massawe, Lyaruu, Makyao, Mowo,
Lamtey, Tairo, Mramba, Kauki
wanatoka Rombo. Sawe, Usiri,
Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa,
Mtui, Moshi, Meela, Minja, Njau
wanatoka Marangu na Kilema.
Rite, Makule, Minja, Mashayo,
Chao, Shao, Makawia, Ndesano,
Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo,
Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia,
Kessy, Mmbando, Matemba,
Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo,
Towo, Mkony, Temba na kadhalika
hutoka Kibosho.Ukoo wa akina Teri
wako Mamba Kiria na wachache
Sango, Old Moshi na wengine
walihamia Maji ya Chai, Mkoa wa
Arusha.
Wachagga wengi hupenda kurudi
nyumbani kipindi cha Krismasi ,
ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao,
rafiki, au ndugu. Ingawa wengi
hudhani kwamba Wachagga
wameathiriwa sana na dini ya
Ukristo kwa kuwa wengi wao ni
Wakristo na hiki huwa ni kipindi
cha likizo kwao, inaaminika pia
kuwa kurudi kwao Uchagani wakati
wa Krismasi ni pamoja na
kutembelea ndugu zao na
kujumuika pamoja katika
kuumaliza mwaka baada ya kazi
nyingi za kutafuta pesa kwa mwaka
mzima.
Utawala wa jadi ya Wachagga
Watawala wa kichagga waliitwa
"Mangi". Hawa walihodhi
mashamba, ngombe na
waliheshimiwa kama viongozi wa
kikabila. Walikuwa na nguvu za
kisiasa na utajiri. Baadhi ya ma-
mangi mashuhuri katika historia ni
kama Mangi Rindi aliyeingia
mikataba na wakoloni
(wajerumani), Mangi Sina wa
kibosho - anajulikana kwa uhodari
wake wa vita katika kupigana na
wamachame na kupora ngombe na
mazao yao na Mangi Marealle wa
Marangu na Vunjo. Wakoloni
walipokuja Kilimanjaro waliingia
mikataba na viongozi hawa wa
kikabila ili kuweza kuweka misingi
yao ya kikoloni. Pia ndugu na
watoto wa ma-Mangi walikuwa wa
kwanza kupata elimu ya kikoloni,
kwa hiyo waliweza kushirikishwa
katika serikali za kwanza. Hawa
pia wanaaminika walikuwa ni kama
mabepari wa kwanza wa ki-jadi,
maana walifanyiwa kazi na watu
wengine wakati wao ma-mangi
wamekaa kuhesabu mali zao.
Usemi maarufu wa "u-Mangi-
meza" nadharia
inawezekana kuwa umetokana na
watawala hawa wa kichagga.
Ardhi
Ingawa ardhi ni msingi wa
maendeleo kwa watu wote, kwa
wachagga, ardhi ni mali sana kwa
sababu kilimo chao ni cha mazao
ya kudumu kama kahawa na ndizi
hukaa shambani kwa muda wa
miaka mingi. Mojawapo ya urithi
wapewayo watoto ni "kihamba".
Hii ni sehemu ya ardhi ambayo
mtoto anategemewa atajenga na
kuanzisha familia yake. Bahati
mbaya watoto wa kike walikuwa
hawapewi kipaumbele katika
ugawanaji wa vihamba. Uhaba wa
ardhi uchagani ulipelekea
wachagga wengi kuhamia mikoa
mingine. Hivi leo utakuta
wachagga wakiishi Dodoma,
Morogoro, Iringa, Mbeya nk wakiwa
wamepanda migomba yao na
kuendesha biashara za maduka ya
vyakula. Ukienda kwenye mikoa hii
utakuta wamejenga jamii zao na
vyama vyao vya kusaidiana wakati
wa sherehe au matatizo. Aidha
hata pombe ya mbege utaweza
kuikuta katika makusanyio ya
wachaga mikoani mbali mbali.
Maoni juu ya Wachagga
Ingawa wanaume wa kichagga
hupendelea kufanya kazi mbali na
kwao, wake zao hukaa nyumbani
(Moshi) na hufuga ngombe na kazi
za shambani. ila kwa sasa
kutokana na ugonjwa wa ukimwi
tabia hii imepungua miongon
mwao. Wanawake wa kichagga
(hasa kutoka Rombo) hujulikana
kama wafanyakazi hodari.
Huchangia sana katika mapato ya
nyumbani na chakula. Ingawa
kipato cha wachaga ni kikubwa
kulinganisha na cha makabila
mengine, takwimu zinaonyesha
watoto wa mkoa wa Kilimanjaro
kuwa kuongoza kwa utapiamlo.
Sababu kubwa ya watoto kuwa na
utapiamlo kunatokana na wazazi
kujali zaidi kazi kuliko muda wa
kuwahudumia watoto. Wengi wa
wototo ni wale ambao wazazi wao
ni watu wapombe na kipato chao
kinaishia kilabuni. Utaona kwamba
uchagani kuna vilabu vingi vya
pombe na vinaongezeka kwa
sababu imekuwa nibiashara
kubwa. Karibu kila kaya kumi
natano kuna kila cha pombe na
kiwango cha chini kabisa cha
pombe inayouzwa kwa siku katika
vilabu hivyo si chini ya dede sita
au lita mia moja. Pombe ni
sababu moja ya watoto kuwa na
utapiamlo Hii inawezekana kuwa
matunda ya wazazi kutowalisha
watoto wao chakula cha kutosha
au chakula bora. Kuna sehemu
nyingine za Uchaggani kama Old
Moshi na Kibosho ambapo watoto
wadogo hupewa pombe ya mbege
asubuhi mchana na jioni. Sababu
nyingi ni kazi; mama wa kichagga
anaweza kushinda shambani kutwa
na hawana desturi ya kubeba
watoto mgongoni kwenda nao
shambani hivyo wanakuwa
nyumbani ama wenyewe au na
mayaya. Mfano ulio dhahiri ni
nyakati za asubuhi na mapema
kwenye vyombo vya usafiri karibu
robo tatu ya abiria ni wanawake
wakienda katika shuguli za
kibiashara na kilimo na vivyo hivyo
nyakati za jioni wakirudi
majumbani. Hao ni nje ya wale
wanaotumia usafiri wa miguu
ambao ni wengi zaidi. Pia baadhi
ya wamama wa kichaga wanawajali
waume zao zaidi kwani nyama
nzuri ni ya baba. Kuepuka
gharama baba ataandaliwa
chakula kizuri tofauti na
chakulawalichoandaliwa watoto
japo ni chakula kilekile.pia
wachaga wamekua na desturi ya
kuwaenzi wazee wao walio tangulia
mbele za haki kwa kuwatambikia
kwa pombe na nyama za mbuzi
pale tu wanapo rudi nyumbani
ifikapo mwezi desemba. hili
limekua ni swala la kawaida sana
na halipingiki. wengi wao huwa
wanarudi na magari ndio sababu
utaona ya kwambwa kila ifikapo
mwezi desemba kila mwaka foleni
za magari zimekua zikiongezeka
kutokana na wachaga kurudi
nyumbani msimu wa sikukuu.
wengi wao wamekua wakitoka
sehemu mbalimbali za nchi na
hata nje ya nchi......imeandaliwa na deo kessy kwa ushirikiano wa vitabu mbalimbali vya historia.....
MAKALA MAALUMU JUU YA WACHAGA IMEANDALIWA NA MMILIKI WA BLOG HII DEOGRATIUS PAUL KESSY TOA MAONI YAKO HAPA +255783150977
Views:
Video Information