Mahakama ya kimataifa ya jinai ICC
imempata na hatia ya uhalifu wa
kivita mbabe wa kivita kutoka
Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo,
Germain Katanga.
Hata hivyo Katanga hakukutwa na
hatia katika shtaka la udhalilishaji
wa kijinsia.
Alituhumiwa kuhusika na mauaji ya
wanavijiji zaidi ya 200 mwaka 2003
katika jimbo la Ituri lenye utajiri wa
dhahabu, kaskazini mashariki mwa
Congo.
Katanga ni mtu wa pili kupatikana
na hatia ya uhalifu wa kivita katika
mahakama ya ICC tangu ianzishwe
mjini The Hague, Uholanzi mwaka
2002.
Katika shambulio hilo lililotokea
mnamo Februari 24, 2003 watu 200
waliuawa katika kijiji cha Bogoro
karibu na mpaka wa Uganda,Katanga
wakati huo akiwa Kamanda wa kundi
la waasi la Patriotic Resistance Force
of Ituri (FRPI) lililotekeleza mauahi
hayo.
Mwendesha mashtaka amesema nia
yao kuu ilikuwa kuangamiza kijiji
kizima.
Germain Katanga kwa jina la utani
Simba alikanusha mashtaka hayo
yote dhidi yake.
Katanga wa DRC matatani.
Views:
Video Information