Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
leo anatarajiwa kuzindua rasmi
shughuli za bunge la kitaifa
kuhusu marekebisho ya katiba
mjini Dodoma katika hatua
itakayoanzisha rasmi mjadala wa
kitaifa kuhusu marekebisho hayo.
Bunge hilo maalum la katiba
limepewa kati ya siku 70 hadi 90
kujadili rasimu ya katiba na kisha
kuifanyia marekebisho kabla ya kura
ya maamuzi.
Kuna ripoti kwamba baadhi ya
wajumbe kutoka upinzani na
mashirika ya kiraia yanapanga
kuvuruga shughuli hiyo ya uzinduzi.
Suala la hotuba ya Rais Kikwete
limekuwa sehemu ya mjadala katika
Bunge hilo kutokana na baadhi ya
wajumbe kuhoji sababu za Jaji
Warioba kuwasilisha Rasimu kabla
ya Rais kuzindua Bunge kwa mujibu
wa kanuni.
Mjadala huo uliwafanya baadhi ya
wajumbe kumzuia Jaji Warioba
Jumatatu iliyopita kuwasilisha
rasimu hiyo kama ilivyokuwa
imepangwa.
Kikao cha maridhiano kilifanyika
siku hiyohiyo usiku na kufikia
mwafaka kwamba Mwenyekiti huyo
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
awasilishe Rasimu ndiposa Rais
aweze kuzindua shughuli ya kujadili
rasimu hiyo kabla ya kura ya maoni.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kurekebisha Katiba...
Views:
Video Information