Video Information
Balozi wa Ukraine katika Umoja wa
Mataifa ameomba kikao cha dharura
cha Baraza la Usalama ili kufanya
kila linalowezekana kuzuwia uvamizi
wa Urusi, wakati vikosi vya jeshi la
nchi hiyo vikidhibiti jimbo la Crimea.
Lakini hatua hazionekani kuwa
zinaweza kuchukuliwa na chombo
hicho chenye nguvu cha Umoja wa
Mataifa. Kama mwanachama wa
kudumu wa Baraza la Usalama, Urusi
ina nguvu za karata ya turufu na
inaweza kuzuwia baraza hilo
kuidhinisha azimio lolote
litakalokosoa ama kuiadhibu nchi
hiyo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Ban Ki-moon, amemtaka Rais
Vladimir Putin katika mazungumzo
kwa njia ya simu "kuanza
mazungumzo ya ana kwa ana na
maafisa wa serikali mjini Kiev."