Video Information
Benzema na Ribbery
Wacheza soka wawili mashuhuri
duniani, wamefikishwa mahakamani mjini Paris Ufaransa kwa kosa la
kufanya ngono na kahaba aliyekuwa na umri mdogo.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 21 sasa hivi,
alisema kwamba,Franck Ribery, mchezaji wa Bayern Munich , alimtumia
kama zawadi wakati wa sherehe za siku yake ya kuzaliwa mwaka 2009.Alisema kuwa pia alilipwa ili afanye ngono na Karim Benzema anayecheza soka yake na klabu ya, Real Madrid.
Kahaba huyo alisema kwamba, aliwaambia wawili, hao kuwa alikuwa mtu mzima wakati huo.
Benzema amekanusha madai ya msichana huyo.
Wachezaji hao wanaweza kufungwa jela miaka mitatu kila mmoja ikiwa watapatikana na hatia.