Video Information
Kwenye Ligi, WBA itatinga Uwanjani chini
ya Kocha mpya kutoka Spain, Pepe Mel, hii ikiwa ndio Mechi yake ya
kwanza kwa Timu yake ambayo ipo Nafasi ya 14 ikiwa na Pointi 21 na
kucheza na Everton ambayo iko juu ikiwa Nafasi ya 6 na ina Pointi 41.
Ushindi kwa Everton utaifanya izipiku Tottenham na Liverpool na kukamata Nafasi ya 4.
Nao WBA wakishinda watapanda hadi Nafasi ya 10 na kuzipiku Stoke City, Norwich City, Hull City na Aston Villa.
Lakini pigo kwa WBA ni kuwa wanatinga
kwenye Mechi hii wakiwa na udhaifu mkubwa wa Mastraika kufuatia kuumia
kwa Victor Anichebe na Stephane Sessegnon na kuhama kwa Shane Long
kwenda Hull City.
Nao Everton itawakosa Majeruhi Antolin Alcaraz na Ross Barkley lakini wanaweza kumtumia Mchezaji wao mpya Aiden McGeady.
Kwenye Mechi ya kwanza ya Ligi Msimu huu
huko Goodison Park Mwezi Agosti, Everton na WBA zilitoka 0-0 lakini
Uwanjani The Hawthorns WBA imewahi kuifunga Everton mara 5 na Sare 4
katika Mechi za Ligi.
CAPITAL ONE CUP-NUSU FAINALI: MARUDIANO
Jumanne Usiku Uwanjani Upton Park, West
Ham itarudiana na Manchester City katika Mechi ya Nusu Fainali ya
Capital One Cup huku City wakiwa mbele kwa Bao 6-0 baada kuitwanga West
Ham Uwanjani Etihad hapo Januari 8.
Jumatano Usiku ni zamu ya Old Trafford
ambako Manchester United wana kibarua cha kukomboa kipigo cha Bao 2-1
walichopewa huko Stadium of Light hapo Januari 7 katika Mechi ya Kwanza
ya Nusu Fainali ya Capital One Cup.
Fainali ya Kombe hili itachezwa Uwanjani
Wembley hapo Machi 2 na Mshindi wake huiwakilisha England kwenye UEFA
EUROPA LIGI Msimu ujao.
Dondoo muhimu:
-Kwenye Nusu Fainali, Goli lla Ugenini
linahesabika tu pale Timu zitakapomaliza Dakika 120 za Mchezo ikiwa
wamekwenda Sare Dakika 90 na kuongezewa Dakika 30 na Timu kubakia
wamefungana kwa Magoli.
Mathalani, ikiwa Man United wataifunga
Sunderland Bao 1-0 ndani ya Dakika 90 kwenye Mechi ya Marudiano, Mechi
hiyo ya Old Trafford itaongezwa Dakika 30 kwani Jumla ya Mabao ni 2-2 na
mpaka kumalizika kwa Mechi Man United ikiwa watabaki washindi kwa Bao
1-0, na hivyo Jumla ya Magoli kuwa 2-2, hapo ndipo hesabu ya Goli la
Ugenini itakuja na Man United kuibuka kidedea.