Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

CHELSEA YAKUBALI KUMUUZA MATA MAN UNITED KWA PAUNI MILIONI 40

Views:
Video Information

Manchester United imeambiwa itoe pauni milioni 40 kama ina nia ya kweli kumnasa kiungo nyota wa Chelsea, Juan Mata.

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho naye amesema milango iko wazi kwa Mata kama anataka kuondoka.

Mourinho ameonyesha imani kubwa kwa William, Oscar na Eden Hazard kuliko Mata.
Mata naye amekuwa akihofia kukosa nafasi katika kikosi cha Hispania kitakachoshiriki Kombe la Dunia kama ataendelea kubaki Chelsea.
Kwa upande wa Kocha wa Man United, David Moyes, ameonyesha ana nia ya kumpata kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi.
Hapa chini ni namna Mata anavyoweza kutengeneza nafasi nyingi zaidi ya wachezaji karibu wote wa Man United.
WWW.SAYARIBLOG.BLOGSPOT.COM
Similar Videos