Video Information
Murphy hajacheza tangu Msimu uliopita na
sasa ameamua kutangaza rasmi kuwa amestaafu kucheza Soka baada ya
kuacha kucheza tangu Mwezi uliopita.
Murphy, mwenye Miaka 36, aliichezea
Liverpool Mechi 249 kati ya Mwaka 1997 na 2004 na kwenye Msimu wa
2000/01 yeye ndie alikuwa nguzo kubwa walipotwaa Kombe la Ligi, FA CUP
na UEFA CUP kwa mpigo.
Mbali ya kuichezea Timu ya Taifa ya
England mara 9, pia amezichezea Klabu za Crewe Alexandra, Charlton
Athletic, Tottenham Hotspur, Fulham na Blackburn Rovers.
Akitoboa habari hizi za kustaafu kwake,
Murphy amesema kupitia Tovuti ya Klabu ya Liverpool: “Huyu ni mimi,
Miaka 20, nimemaliza. Nilikuwa na maisha mazuri ya Soka na
nitayafurahia.”
Murphy na Klabu yake ya mwisho,
Blackburn Rovers, kabla Msimu huu mpya kuanza, walifikia makubaliano ya
kuvunja Mkataba kati yao.
Murphy amesema: “Kumekuwa na taarifa
kwenye Vyombo vya Habari zikiuliza kama bado nacheza au nipo lakini
niliamua muda nyuma kuwa sasa nastaafu lakini sikutangaza rasmi. Sasa
natangaza rasmi!”