Video Information
MABINGWA wa LIGI 1 huko France, Paris St
Germain, wamepaa kileleni kwa ushindi hapo Jana huku Mbrazil Lucas
Moura akipiga Bao lake la kwanza na kwenye Bundesliga, Hertha Berlin
Jana ilijikuta ikipokea kipigo cha kwanza cha Nyumbani tangu Aprili
2012.
SOMA ZAIDI:
BUNDESLIGA: HERTHA BERLIN 0 STUTTGART 1
Katika Mechi pekee iliyochezwa kwenye
Bundesliga hapo Jana ndani ya Olympiastadion na kushuhudiwa na Mashabiki
46,624, Wenyeji Hertha Berlin walipokea kipigo chao cha kwanza cha
Nyumbani tangu Aprili 2012 walipofungwa Bao 1-0 na Stuttgart.
MSIMAMO-Timu za Juu:
|
NA |
TIMU |
MECHI |
POINTI |
|
1 |
Borussia Dortmund |
4 |
12 |
|
2 |
Bayern Munich |
4 |
10 |
|
3 |
Bayer Leverkusen |
4 |
9 |
|
4 |
Hannover 96 |
4 |
9 |
|
5 |
Mainz |
4 |
9 |
|
6 |
Hertha Berlin |
5 |
7 |
|
7 |
Stuttgart |
5 |
6 |
|
8 |
Borussia Monchengladbach |
4 |
6 |
|
9 |
Wolfsburg |
4 |
6 |
|
10 |
Werder Bremen |
4 |
6 |
Bao pekee la Mechi hiyo lilifungwa
katika Dakika ya 49 na Christian Gentner na kuwapa Stuttgart ushindi wao
wa pili mfululizo tangu wamtimue Kocha Thomas Schneider na kumsimika
Bruno Labbadia.
RATIBA/MATOKEO:
BUNDESLIGA
Ijumaa Septemba 13
Hertha Berlin 0 VfB Stuttgart 1
[Saa za Bongo]
Jumamosi Septemba 14
16:30 Bayer 04 Leverkusen v VfL Wolfsburg
16:30 Bayern Munich v Hannover 96
16:30 SV Werder Bremen v Eintracht Frankfurt
16:30 FSV Mainz 05 v Schalke 04
16:30 FC Augsburg v SC Freiburg
19:30 BV Borussia Dortmund v Hamburger SV
Jumapili Septemba 15
16:30 TSG Hoffenheim v Borussia Mönchengladbach
18:30 Eintr. Braunschweig v FC Nuremberg
LUCAS MOURA AMALIZA UKAME WA MAGOLI, PSG KILELENI!
MCHEZAJI wa Brazil, Lucas Moura, Jana
alifunga Bao lake la kwanza kwa Paris St Germain na kuwasaidia Mabingwa
hao wa France kupaa kileleni mwa Ligi 1 baada ya kuifunga Girondins
Bordeaux Bao 2-0 Ugenini ndani ya Chaban Delmas.
MSIMAMO-Timu za Juu:
|
NA |
TIMU |
MECHI |
POINTI |
|
1 |
PSG |
5 |
11 |
|
2 |
Monaco |
4 |
10 |
|
3 |
Marseille |
4 |
9 |
|
4 |
St Etienne |
4 |
9 |
|
5 |
Rennes |
4 |
7 |
|
6 |
Reims |
4 |
7 |
|
7 |
Lille |
4 |
7 |
|
8 |
Lyon |
4 |
6 |
|
9 |
Bastia |
4 |
6 |
|
10 |
Lorient |
4 |
6 |
Lucas Moura alijiunga na PSG Januari Mwaka huu akitokea Klabu ya kwao Brazil Sao Paulo.
Katika Mechi hii, PSG walifunga Bao la
kwanza kupitia Blaise Matuidi katika Dakika ya 30 na Moura kupiga la
Pili katika Dakika ya 64.