Video Information
Mabingwa Watetezi, Yanga, wako huko
Mbeya kucheza kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine dhidi ya Mbeya
City, Timu iliyopanda Daraja Msimu huu.
Katika Mechi mbili za Ligi walizocheza,
Yanga walianza kwa kuifunga Ashanti United 5-1 na kutoka Sare 1-1 na
Coastal Union wakati Mbeya City walitoka Sare 0-0 na Kagera Sugar na
kuifunga Ruvu Shootinga Bao 2-1.
Vigogo wa Soka Nchini, Simba, wao
watacheza Jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Msimu huu
kwa kucheza Uwanja wa Taifa na Timu kali ya Mtibwa Sugar, ambayo imeanza
kwa ushindi na Sare kama Simba ambayo ilitoka 2-2 na Rhino Rangers na
kisha kuitungua JKT Oljoro Bao 1-0.
Viingilio kwa Mechi hii ya Simba na
Mtibwa Sugar ni Shilingi 5,000 Viti vya Bluu na Kijani, Sh. 8,000 Viti
vya Rangi ya Chungwa, Sh. 15,000 VIP C na B wakati VIP A itakuwa Sh.
20,000.
Nao Azam Fc, ambao Msimu uliopita
walimaliza Nafasi ya Pili nyuma ya Mabingwa Yanga na kuiacha Simba
ikamate Nafasi ya Tatu, ipo Ugenini huko Kaitaba Stadium kucheza na
Kagera Sugar.
Vinara wa Ligi, JKT Ruvu, Timu pekee
iliyoshinda Mechi zake zote mbili za Ligi, watakuwa kwenye Viunga vya
Jiji la Dar es Salaam Uwanja wa Azam Complex kucheza na Ashanti United
ambayo imepanda Daraja Msimu huu lakini hadi sasa hali yao ni taabani
baada ya kuchapwa Mechi zote mbili mfululizo.
VPL-MSIMAMO:
|
NA |
TIMU |
P |
W |
D |
L |
GD |
PTS |
|
1 |
JKT Ruvu |
2 |
2 |
0 |
0 |
5 |
6 |
|
2 |
Yanga SC |
2 |
1 |
1 |
0 |
4 |
4 |
|
3 |
Azam FC |
2 |
1 |
1 |
0 |
2 |
4 |
|
4 |
Coastal Union |
2 |
1 |
1 |
0 |
2 |
4 |
|
5 |
Mtibwa Sugar |
2 |
1 |
1 |
0 |
1 |
4 |
|
6 |
Simba SC |
2 |
1 |
1 |
0 |
1 |
4 |
|
7 |
Mbeya City |
2 |
1 |
1 |
0 |
1 |
4 |
|
8 |
Ruvu Shooting |
2 |
1 |
0 |
1 |
2 |
3 |
|
9 |
Mgambo Shooting |
2 |
1 |
0 |
1 |
-1 |
3 |
|
10 |
Kagera Sugar |
2 |
0 |
1 |
1 |
-1 |
1 |
|
11 |
Rhino Rangers |
2 |
0 |
1 |
1 |
-2 |
1 |
|
12 |
JKT Oljoro |
2 |
0 |
0 |
2 |
-3 |
0 |
|
13 |
Ashanti UTD |
2 |
0 |
0 |
2 |
-5 |
0 |
|
14 |
Prisons FC |
2 |
0 |
0 |
2 |
-6 |
0 |
**MSIMAMO TOKA TFF
VPL: LIGI KUU VODACOM
MATOKEO:
Jumamosi Agosti 24
Yanga 5 Ashanti 1
Mtibwa Sugar 1 Azam FC 1
JKT Oljoro 0 Coastal Union 2
Mgambo JKT 0 JKT Ruvu 2
Mbeya City 0 Kagera Sugar 0
Ruvu Shooting 3 Prisons 0
Rhino Rangers 2 Simba 2
Jumatano Agosti 28
Mtibwa Sugar 1 Kagera Sugar 0
Rhino Rangers 0 Azam FC 2
Mbeya City 2 Ruvu Shootings 1
Mgambo JKT 1 Ashanti United 0
JKT Oljoro 0 Simba 1
Yanga 1 Coastal Union 1
JKT Ruvu 3 Prisons 0