Video Information
CHAMA cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Tume ya Mabadiliko ya Katiba
inayoongozwa na Jaji mstaafu, Joseph Warioba, inawatakia mema Watanzania
hivyo iungwe mkono.
Chama hicho
kimesema Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakitaki mabadiliko hapa nchini
ndiyo maana kinabeza na kimejipanga kukwamisha baadhi ya mapendekezo
yaliyomo kwenye rasimu ya Katiba mpya.
Kauli hiyo
ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk.
Willibrod Slaa, katika mikutano ya mabaraza ya wazi ya Katiba mpya.
Alisema
viongozi na makada wa CCM wamekuwa wakiibeza rasimu hiyo iliyotolewa na
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Joseph Warioba kwa kuihofia
kuwa inakiondoa madarakani chama chao.
