Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

"KUDHIBITI MAAMBIKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO INAWEZEKANA"Dr.KWAYI

Views:
Video Information

                                                BAADHI YA MANESI WAKITOA HUDUMA KWA MTOTO KATIKA HOSPITALI YA ELIZABETH JIJINI ARUSHA.


 RAISI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR.JAKAYA AKISALIMIA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA ELIZABETH JIJINI ARUSHA.


RAIS KIKWETE AKIMSALIMIA MTOTO NA MAMA YAKE KATIKA WODI YA WATOTO.


Mpango wa kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto umeonyesha mafanikio makubwa ambapo takwimu za kitaifa za mwaka 2012 zinaonyesha kuwa yameshuka hadi asilimia tano nukta moja.

Mafanikio hayo yamehafikiwa kutokana na ushirikiano kati ya serikali na wadau mbalilimbali likiwemo shirika la kimataifa lisilo la kiserikali la ELIZABETH GRASCER PEDRIADRICK AIDS FOUNDATION

Mganga mkuu wa hospitali ya Mt.ELIZABETH jijini Arusha Dr. TOMATH KWAYI amesema kuwa shirika hilo limetoa huduma kwa wakina mama wajawazito 871 tangu mwaka 2009 lilipo anza kutoa huduma hiyo ambapo watoto saba tu ndiyo walio zaliwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Mkurugenzi wake hapa nchini Dr. CRISPIN KIMARIO amesema katika mikoa sita ambayo shirika hilo limetekeleza mpango huo kwa kipindi cha miaka kumi sasa shirika limefanikiwa kuwahudumia zaidi ya wakina mama wajawazito milioni mbili.

Pamoja na hayo watoa huduma hizo wamesema mafanikio yangekua makubwa zaidi kama walengwa wangekabiliana na  changamoto za  kukatisha kutumia dawa kutokana na imani potofu ikiwemo ya kufuata huduma za waganga wa jadi.

Similar Videos