Video Information
Bila
shaka hali hii ndiyo inayowatisha CCM na kuwakatisha tamaa kabisa.
Wananchi kwa vitendo wameendelea kuiasi na kuikataa CCM na vitisho vyake
vyote, ikiwemo vya kuwatumia baadhi ya mabosi wa Jeshi la Polisi,
kufanya hujuma dhidi ya Vuguvugu la Mabadiliko, ambapo hivi karibuni
imeshuhudiwa ikifikia hali mbaya zaidi pale 'wahujumu' walipoamua
kutumia mabomu ya machozi, mabomu ya kivita na bunduki za kivita zenye
risasi za moto!
Wananchi wameendelea kusimama na upande unaowatetea, kuwasemea na kuwawakilisha. Wamesimama upande wa watetezi wa haki, wapinga dhuluma.
Moja ya malengo ya hujuma za hivi karibuni ilikuwa ni kuwatisha wananchi waogope kuhudhuria mikutano ya CHADEMA. Imeshindikana. Watanzania wameshaamua kusonga mbele. Hakuna kitakachowarudisha nyuma katika kuisaka haki, kutafuta mabadiliko ya utawala na mfumo.

Mkutano wa kwanza wa CHADEMA mara baada ya shambulio la kigaidi la bomu
pale Soweto, Arusha, ulifanyika Songea, ikafuatiwa na Shinyanga, kisha
Tabora, ikiwa ni shughuli za ukamilishaji wa kuzindua Kanda ya Kusini
(Ruvuma, Mtwara na Lindi) Kanda ya Ziwa Mashariki (Simiyu, Shinyanga na
Mara) na Kanda ya Magharibi (Kigoma, Tabora na Katavi).
Kote huko wananchi, Watanzania wote, bila kujali tofauti zao, za kisiasa, kiuchumi na kijamii, wameendelea kuunganishwa na matatizo yao ya msingi kama jamii moja, iliyokwamishwa na kunyimwa fursa ya kuendelea, kutokana na uongozi mbovu wa CCM, uliokumbatia ufisadi, ubadhirifu, dhuluma kwa wananchi walioiamini hapo kabla na sasa umeanza kuwagawanya kwa sera zinazopalilia ubaguzi wa dini, ukanda na ukabila.
Ushahidi wa picha, ambazo zinaonesha wananchi wa maeneo mbalimbali, maelfu kwa maelfu wakisikiliza hoja na kushiriki kwenye Mabaraza ya Wazi ya CHADEMA, kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya, unapaswa kuwa somo kubwa kwa CCM na vibaraka wao wachache kwenye vyombo vya dola, ambao wameamua kutumika na kutia doa majeshi yetu na askari wetu wengine (wengi) waaminifu na watiifu kwa wananchi wanaopaswa kuwatumikia kwa kutenda na kulinda haki kwa kufuata katiba, sheria, kanuni na taratibu za nchi.
Picha; wananchi walivyoipokea CHADEMA, utoaji wa maoni yao Rasimu ya Katiba Mpya;
Hapa ni mikutano ya jana kuanzia Njombe, Makambako, Ilula na Iringa mjini...