Video Information
Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Kati, Usharika wa
Segerea Wilaya ya Ilala, limechomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa
kuamkia jana.Tukio hilo lilitokea saa saba usiku, wakati waumini wa kanisa hilo wakiwa katika mkesha wa maombi ya maandalizi ya mkutano wa injili unaoanza leo.
Mchungaji
wa kanisa hilo, Noah Kipingu alisema wakati wakiwa katika maombi ghafla
walisikia sauti ya kitu kilichorushwa kutoka nje ya kanisa kikiambatana
na moto, ambapo kilianguka madhabahuni na kuanza kuunguza baadhi ya
vifaa vya kanisa.
“Tukiwa
tumesimama mbele ya madhabahu kwa njia ya mduara ndipo nyuma ya
madhabahu ukatokea mlipuko mkubwa kwa sauti ya kishindo, na moto
ukatanda madhabahu,” alisema Kipingu na kuongeza kuwa:
“Katika namna ya kibinadamu hakuna aliyeweza kuvumilia, kila mtu alikimbia akitafuta namna ya kujiokoa.”
Kipingu
alisema kuwa alipobaini kuwa ulikuwa ni moto wa mafuta aliwaambia
waumini wake waingie ndani kwa ajili ya kuuzima, wakati wakiuzima moto
huo walipata taarifa kuwa gari la Mchungaji, Toyota Cresta lenye namba
za usajili T 482BAF lililokuwa nje ya kanisa lilikuwa likiwaka moto.
“Baadhi
ya waumini waliokuwa ndani walikwenda nje kushirikiana na mlinzi
kuuzima moto huo, tunamshukuru Mungu kwamba matukio yote mawili
tumeyashinda kwa uwezo wake,” alisema.
Kipingu alisema kuwa shambulizi hilo lilizua taharuki kubwa kwa waumini wake, na kwamba baadhi ya watu waliwaona watu wanne wakikimbia kutoka eneo la kanisa baada ya kutukio hilo.
Shukuru
Thobias mmoja wa waumini waliokuwepo kanisani wakati tukio hilo
likitokea, anasema aliona vitu kama mshale vikianguka madhabahuni na
vilipodondoka vililipuka kama moto.
“Moto ulianza kuunguza Biblia na makapeti, ndipo tukaanza kukimbia kwenda nje kuchukua mchanga na kuanza kuuzima.
"Baada
ya hapo tulianza kukimbia huku wengine wakidondoka na kujeruhiwa kidogo
miguuni. Niliporudi baadaye niligundua zilikuwa ni chupa tatu za bia
zilizokuwa zimetengenezwa bomu la petroli,” alisema Thobias.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo hakuna mtu aliyepoteza
maisha na kulitaja kuwa ni jaribio la kiharifu lililoshindwa.
“Hakuna
mtu aliyepoteza maisha, lilikuwa jaribio ambalo halikufanikiwa. Wakati
tukio linatokea waumini walikuwa kanisani kwa hiyo waliwahi kuuzima moto
kabla haujaleta madhara,” alisema Kova.
Matukio ya makanisa kuchomwa moto
Mei
26, 2012, Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo Mtaa wa
Kariakoo mjini Unguja, lilichomwa moto usiku na watu wasiofahamika
