Video Information
Ni sawa tunafahamu Ice Prince wa Nigeria ndio mshindi wa tuzo ya BET mwaka huu akiwa anatoka Afrika lakini kitu ambacho unaambiwa ni historia, ni pale BET Awards mwaka huu walipoamua kubadili utaratibu sio kama wakati uliopita ambapo msanii wa Afrika alikua haonekani kwenye stage kama wasanii wa Marekani wanaotangazwa washindi.
Ilikua ni kwenye kichumba kidogo tu akishashinda anaitwa na kuhojiwa pale ila this time Ice Prince amepata zali la kuonekana na audience ambayo kwake ni nafasi nzuri kwa sababu amepewa nafasi sawa na wasanii wa Marekani, Ice alifurahi mpaka na akasema hiyo tuzo sio yake peke yake.
Akaamua kuwaita wale wasanii wengine wa Afrika waliokua pamoja kwenye category moja kama kina Radio na Weasel wa Uganda, Donald na Toya wa South Africa na kusema hiyo tuzo ni ya wao wote, ni ya Afrika…. ilikua poa sana!