Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

HIKI NDICHO WALICHO KISEMA CHADEMA KUPITIA MTANDAO WA KIJAMII FACEBOOK LEO 4/07/2013

Views:
Video Information
Chadema in Blood
Sasa ni wazi kuwa CCM kwa kushirikiana na serikali na vyombo vya dola wamepanga kuhakikisha uchaguzi wa Arusha uliopangwa kufanyika 14/June/2013 unavurugwa na kuhairishwa kwa muda mrefu. Mpaka sasa uchaguzi huo umeshahairishwa mara mbili lakini pia hapo kabla ulishachelewa sana kuitishwa.
Mipango kadhaa miovu imeshafanyika na mingine inaendelea kufanyika chini kwa chini ili kuleta hali ya taharuki na fujo ili kujenga sababu ya kuufuta uchaguzi wa madiwani Arusha. Baadhi ya mipango ambayo tayari nimeipata kutoka chanzo cha ndani cha vyombo vya dola na CCM ni hii:
1/Kuleta maandamano siku ya Ijumaa ya 'Madereva wa Noah' ya kumpinga Lema na hapo hapo kutengeneza kikundi kingine cha watu ili kionekane kuyaingilia maandamano hayo, kisha ijengwe taswira kuwa kuna fujo Arusha.(Mwanzoni ilikuwa wazee wa kimila wa kimasai(Lweugwanani) watumike kutaka kufanya maandamano hayo)
2/Wakina mama na wamachinga wanaofanya biashara kwenye barabara na masoko kadhaa ya Arusha huenda watatimuliwa na mgambo wa jiji la Arusha wiki ijayo ili kutengeneza mazingira ya fujo mjini.
3/Huenda Viongozi wa Chadema mkoani Arusha hususani Lema wakakamatwa na Polisi katika mazingira ya kutatanisha(Itadaiwa wanafanya kampeni nk.) na hapo wananchi wapate hasira na kuanzisha ghasia kutaka kuachiliwa kwao.
4/Kuna mipango ya hujuma ya Kuanzisha matukio maovu kama Moto usiku, yanadaiwa kupangwa na vyombo vya dola kwenye maeneo ya masoko, majengo kadhaa mjini Arusha hususani yenye shughuli nyingi za kibiashara.
Mipango yote hiyo miovu kwa sasa inaratibiwa na CCM taifa chini ya usimamizi wa mkuu wa mkoa wa Arusha Mulongo na kada wa CCM Kijuso.
5/Baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM na serikali wanaishinikiza Tume ya Uchaguzi kuhairisha uchaguzi huo kwa muda usiojulikana hata kama hakuna sababu yoyote ya msingi, kwa kutumia Lugha kuwa ''Uchaguzi utafanyika muda muafaka utapofika''
Similar Videos