Video Information
Utabiri huo ulitolewa na baadhi ya wananchi wanaofuatilia vikao hivyo baada ya kuwaona wabunge kadhaa wa CUF wakija juu ukumbini wakidai hotuba hiyo isitishwe mpaka maneno kuwa CUF kinaunga mkono ndoa ya jinsi moja yatakapoondolewa.
Naibu Spika, Job Ndugai ilibidi aamuru Kamati ya Maadili ya Bunge ikutane mara moja kupitia hotuba hiyo na kusogeza mbele muda wa bunge.
Tukio hilo siyo la kwanza, hivi karibuni nje ya Ukumbi wa Bunge kulizuka tafrani baada ya wabunge wa CCM wakiongozwa na Profesa Juma Kapuya kukasirishwa na kitendo cha mwenzao wa Nkasi Kaskazini, Ali Keisy kupinga Bajeti ya Wizara ya Ujenzi wakati akichangia hotuba ya wizara hiyo kwa madai kuwa haungi mkono hoja kwa sababu barabara ya Sumbawanga hadi Kanazi-Mpanda mpaka Kibaoni haijajengwa kwa kiwango cha lami.
Hali kama hiyo ilijitokeza tena Mei 20, mwaka huu nje ya ukumbi baina ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela.
Mtafaruku huo uliibuka baada ya Kilango kusikika akimtuhumu Lissu kwa uchochezi, akisema kwamba amekuwa mbunge pekee anayeongoza kwa vurugu, maneno ambayo hayakumfurahisha Lissu ambaye alishindwa kuvumilia na kumgeukia (Kilango) kwa nguvu huku baadhi ya wabunge wakishuhudia na wengine wakimzuia.
Wabunge wanapaswa kuvumiliana na kubishana kwa hoja la sivyo wanaweza kusababisha amani kuvunjika ndani ya bunge lao tukufu- Mhariri.
Source:Global Publisher
