Video Information
Watu wengi sana tumezoea kuona migogoro ya ardi ikiwa ni
makabila kwa makabila lakini imeonekana kutokea kwa migogoro kati ya ndugu kwa
ndugu .
Ilikuwa ni jumamosi ya tarehe 09-02-2013 kulikuwa na mkutano
mkubwa ambao ulikutanisha baadhi ya viongozi wa kijiji pamoja na viongozi wa
ukoo.mwenyekiti wa ukoo alikuwa ni Philip Tesha na mwenyekiti wa kijiji alikuwa
ndugu Eleutery Swaty kuhakikisha ndugu hao wamepatana.
JINSI
ILIVYO KUWA MWANZO HADI MWISHO
Upatikanaji
wa shamba Laurenti Tesha aliweza kumpatia Michaeli tesha shamba kama ndugu yake
lakini alitokea ndugu mwingine ambaye ni Faustine Tesha akamwambia eneo ambalo
umepewa sio sahihi kwa wewe kuishi kwani lilikuwa ni eneo la bondeni na
kumpatia nkipande cha eneo.
Kwa upande wa
mlalamikaji ambaye ni familia ya Faustine Tesha wamesema eneo hilo alipewa kwa
muda hadi atakapo pata eneo rasmi la kuishi lakini hakuna maandishi ambayo
yanaonyesha makabidhiano.tangu mwaka 1979 ndiyomwaka ambao waliweza kupeana
eneo hilo la shamba na pia hakuna
maandishi yanayothibitisha hilo.
Pia inaonekana
chanzo cha mogogoro hiyo inasemekana ni mlalamikiwa Michael Tesha kutengeneza
msingi wa nyumba na walalamikaji kusema kuwa amesogeza mpaka wa shamba lao na
kutaka kumfukuza katika eneo alilopewa na marehemu ndugu yake Faustine Tesha.
Wakati kikao
kinaendelea ilifika mahali kukatawaliwa na hasira kwa upande wa walalamikaji
ndipo mwenyekiti wa kijiji cha Njari Eleutery Swaty akawanyamazisha na
kurudisha hali ya utulivu pamoja na amani na kuweza kuendelea na kikao.
Ilionekana wazi
kuwa familia ya Faustine Tesha kwenda
kupanda migomba pamoja na kahawa katika eneo alilopewa Michael Tesha na ni
karibu na nymba yake anayoishi kwa sasa ambayo mtoto wa Michael anataka kujenga
nyumba.
Chanzo kingine
ambacho kimeonekana ni ndugu Michael hajawahi kutoa hata kitu kwa familia ya
Faustine na kuonyesha kama shukrani kwa kupewa eneo la kuishi pia marehemu
faustine alipofariki hakuna aliye kwenda kutoa neno lolote kama kuna sehemu kapewa
na marehemu na amefariki itakuaje.
Kikao kilifanyika
mbali na eneo la tukio na kulazimu aliye kuwepo pale kwenye kikao kwenda
kuangalia eneo wanalo gombania .Vilevile kulikuwa na barua batili ya kuonyesha
kikao cha ukoo wa Tesha pamoja na mwenyekiti feki aliye kuwa amesaini barua
hiyo amabaye ni William Tesha na barua hiyo dhahiri shahiri ilonekana kuegemea
upande mmoja.
Pia eneo
wanalogombania awamu Michael alikuwa ametengeneza nyumba ya ng”ombe na ndipo
alibomoa kwa ajili ya kujenga nyumba ya mwanaye.Na mwenyekiti wa kijiji aliweza
kusema kuwa kama hawataki aishi eneo hilo waweze kumfidia lakini hakuna aliye
afiki kitendo hicho.
Baada ya
ukweli kuonekana familia ya Faustine waliweza kusema kuwa wamemwachia eneo hilo
na pi mwenyezi mungu aangalie kama ni haki huku ikiwa ni kwa shingo upande siyo
kwa nia nzuri wala moyo mmoja.
MWISHO kikao
kilimalizika kwa uongozi wa kijiji kumwambia Michaeli aweze kuita baraza la
ardhi kwaajili ya kuweka mipaka sahihi ili kuepusha usumbufu na kuishi katika
eneo lake bila matatizo yoyote na endapo kuna tatizo litakalo jitikeza aweze
kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji.
DEOGRATIUS KESSY