Video Information
Maandamano ya wananchi wanaotaka usalama Mali
Baraza la usalama la Umoja wa
mataifa limetoa wito wa kupelekwa kwa wanajeshi wa kimataifa nchini Mali
ambako wapiganaji wa kiisilamu wadai wameuteka mji muhimu wa Konna.
Wakati huohuo, duru za kidiplomasia zinasema
kuwa rais wa Mali ametoa wito kwa Ufaransa kusaidia katika kupambana na
wapiganaji hao, hoja iliyojadiliwa katika mkutano wa dharura wa baraza
la usalama la umoja wa mataifa.Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice, alihoji ikiwa rais Dioncounda Traore alikuwa ametoa ombi maalum na kufafanua aina ya msaada anaotaka.
Ufaransa inatarajiwa kutoa jibu lake leo wakati wa mkutano wa dharura utakaofanyika , kwa mujibu wa balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, Gerard Araud.
Wapiganaji wa Mali walioteka mji mwingine mpya wa Konna
Wapiganaji wa kiisilamu wameweka sheria kali za kiisilamu katika eneo hilo.
Kwa sababu ya mipango ya usafiri na vifaa , kikosi cha wanajeshi wa Afrika hakitatarajiwa kuanza kazi hadi ifikapo Septemba au Oktoba.