Video Information
Wawakilishi wa Wakala wa Kimataifa
wa Nishati ya Atomiki IAEA wamewasili Tehran. Wawakilishi wa IAEA
ukiongozwa na Herman Nackaerts Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa
Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia alfajiri ya leo wamewasili hapa mjini
Tehran. Kwa mujibu wa ripoti hiyo ujumbe wa IAEA umepokelewa na Ali
Asghar Sultaniye Mwakilishi wa Iran katika wakala wa IAEA. Wawakilishi
wa IAEA kesho watakuwa na mazungumzo ya kiufundi na maafisa wa nyuklia
wa Iran na pande mbili hizo zitajadili na kubadilishana mawazo kuhusu
kadhia ya nyuklia. Duru ya sita ya mazungumzo ya Iran na wakala wa IAEA
ilifanyika hapa Tehran tarehe 13 Disemba mwaka jana.