Video Information

YeS..ni
Climax Bibo, Star kutoka 'kruu' ya Mexicana Lacavela, ambaye
amedondosha 'single' mpya akiwa ndani ya Record Lebo mpya ya BML
chini ya mkali kitambo kwenye 'game' Benjamin Busungu a.k.a Benjamin
wa Mambo Jambo.
Akipiga stori na teentz.com, juzi kati, Climax alifunguka kuwa
ngoma hiyo mpya inakwenda kwa jina la 'Getho Boy' tayari
imeshafanyiwa mpango wa Video na soon itakuwa kwa hewa mara baada ya
kumalizika kwa zoezi la kuifanyia Editing.
"Nashukuru Mungu huu ni ujio wangu mpya nikiwa kwenye mikono ya
BML, binafsi namkubali sana Benja na ninajua tutapiga bao kwa kile
tunachokifanya sasa, kikubwa naomba fans kuipokea ngoma hiyo na
kuyapitia mashairi ili kuyaelewa zaidi kupitia clip yake hapo chini"
alisema Climax
Kwa upande wake C.e.o wa BML Production, Benjamini wa Mambo
Jambo, amedokeza kuwa ngoma hiyo ya Climax 'Getho Boy' pia itatumika
kama Soundtrack kwenye movie ya Coast to Coast iliyoigizwa na mkali
Slim Omary aliyecheza na mastaa wengine kibao kama Yussuph Mlela, Hemed
Suleiman 'PHD' na mwandada Angel ambayo nayo pia Soon itakuwa mtaani.