Video Information
Ivory Coast inajiandaa kuanza kampeini yao katika kinyanganyiro cha kuwania kombe la mataifa ya Afrika siku ya Jumatatu dhidi ya Togo.
Kocha wa Ivory Coast, Sabri Lamouchi, amesema kikosi chake kiko tayari kujaribu kufuta matokeo ya mwaka uliopita ambapo walishindwa katika mechi ya fainali na Zambia.
Timu hiyo ambayo imeorodheshwa timu bora zaidi barani Afrika, itakuwa na kibarua kigumu, kudhihirisha kuwa wao wana uwezo wa kutwaa kombe hilo mwaka huu, hasa baada ya kushinda kulitwaa katika mashindano manne yaliyopita.
Mwaka wa 2006 na mwaka uliopita, Ivory Coast, ilishindwa kwenye fainali kupitia mikwaju ya penalti na Misri na Zambia mtawalia.
Kocha huyo amesema wamejiandaa vilivyo na wako tayari kwa mechi yao ya kwanza.
Ila amekiri watakuwa na shinikizo chungu nzima kuandikisha matokeo mema.
Ivory Coast, ilishinda kombe hilo mara ya mwisho miaka 20 iliyopita.
Kocha huyo kutoka Ufaransa amesema licha ya wao kucheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Misri, kikosi chake kiko katika hali nzuri.
Ivory Coast, ilishinda mechi hiyo kuwa kuilaza Misri Magoli 4-2, katika mechi iliyochezwa mjini Abu Dhahi.
Baada ya Togo, Ivory Coast, chini ya naodha wake Didier Drogba, itachuana na Tunisia na Algeria.