Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

PICHA NA TAARIFA ZA VURUGU ZINAZOENDELEA KIBITI RUFIJI SASA HIVI, WANANCHI WAMEVAMIA POLISI.. WANACHOMA

Views:
Video Information
.
Mwandishi Mrokim wa Father Kidevu Blog anaripoti kwamba kundi la wananchi wenye hasira wamevamia kituo cha Polisi Kibiti Wilayani Rufiji na kuleta vurugu kubwa kutokana na raia mmoja kufa kwa kile kilichodaiwa kuwa kipigo cha Polisi.
Aliyefariki ni Hamis Mpondi ambaye mauti yamemfika wakati akipatiwa matibabu Muhimbili.
Habari za sasa ni kwamba wananchi hao wanateketeza nyumba za Askari Polisi  zilizopo jirani na kituo hicho licha ya juhudi za Polisi kuwatawanya kwa mabomu, pia wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe magogo na kuchoma matairi ikiwa ni umbali wa kama kilometa moja kutoka kituo cha Polisi Kibiti, hali inaelezwa kuwa inazidi kuwa tete huku Polisi wa Kibiti wakiendelea na jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua mabomu hewani kujaribu kutawanya watu
Similar Videos