Video Information
Ukizungumzia mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya mwenye sauti ya pekee (Personal Identity) mwenye mashairi yaliokwenda shule na yanayogusa hisia na maisha ya kawaida ya kila siku hasa kwenye maswala ya mapenzi ….
Na inasemekana ni msanii anayeongoza kwa kupendwa na wanandoa wengi hapa bongo kutokana na jinsi mashairi yake yanavyowagusa hasa wanandoa ndani ya nyumba…..ni msanii pekee wa bongo fleva ambaye anawagusa sana watu wazima kuliko msanii mwingine yeyote wa bongo fleva………. na si mwingine ni Linex ..!….. hivi punde tu ametoka kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la MAHAKAMA YA MAPENZ
Wimbo umetengenezwa Sweden kwa Fundi samweli sauti imerekodiwa na Tuddy Thomas, kwahiyo uandaaji mzima wa wimbo umefanywa na producer Fundi samweli (mzungu)