Video Information
Nahodha wa Ivory Coast Didier Drogba
Kundi D leo linakamilisha
mzunguko wa pili kwa timu 16 zinazowania taji la ubingwa wa Kombe la
Afrika barani Afrika kwa mwaka 2013.
Ivory Coast kwa sasa inacheza na Tunisia katika
mchezo wa kwanza wa kundi hilo na kufuatiwa baadaye na Algeria
itakayokuwa ikipambana na Togo.Kufikia sasa Ivory Coast 1 Tunisia 0.
Bao hilo lilifungwa kunako dakika ya 19 na mshambuliaji wake Gervinho.
Ivory Coast sasa ina alama sita katika kundi hilo baada ya kushinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Togo.
Tunisia ina kikosi imara kitakachopigana kuwaangusha miamba hao wa soka barani Afrika.
Tunisia imekuwa ikishiriki mara kwa mara katika fainali za Kombe la Afrika, Lakini wamefanikiwa mara moja tu kutwaa kombe hilo ilipoandaa michuano hiyo mwaka 2004.
Wachezaji wa Tunisia
Kocha wa Tunisia Sami Trabelsi ni kipenzi cha mashabiki nchini Tunisia akiwa mchezaji maarufu wa sehemu ya ulinzi katika timu ya taifa, akishiriki katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka1996 na 2000, pamoja na zile za mwaka 1998 nchini Ufaransa.
Ivory Coast inajivunia nyota wake kadhaa wanaosakata kabumbu ndani na nje ya nchi hiyo.
Miongoni mwao ni Didier Drogba anayechezea nchini Uchina, Yahya Toure, mchezaji bora wa soka barani Afrika mwaka 2013 na pia tegemeo la timu ya Manchester City ya England, Wengine pamoja na timu wanazochezea kwenye mabano: