Video Information
0
Imefahamika kwamba zaidi ya
wafungwa 700 raia wa Nigeria ambao wamefungwa kwenye magereza mbalimbali
nchini China wameomba msaada wa rais wao Goodluck Jonathan kuwakomboa
waondokane na mateso wanayopata.
Wengi wamelalamika marafiki zao na ndugu zao kufungwa kwenye magereza mbalimbali kutokana na kuisha muda wa documents za kusafiria, na kuna wengine wanasema hawajui sababu za kukamatwa kwao.
Imeripotiwa na NGT kwamba ni zaidi ya Wanigeria 1000 waliofungwa toka december25 2011.
Mfungwa mmoja wa Kinigeria aitwae Paul amekaririwa na Sunday Sun akisema “tunateswa sana, chakula hakina ladha hapa, hali ni mbaya sana… hata ukiumwa haupelekwi hospitali, hali ni mbaya ninavyokwambia ndugu yangu… ni mbaya sana! tunachoomba ni rais wetu aje kutuokoa, kuna sheria mpya sasa hivi kwa nchi za nje kuja kuchukua wafungwa wao na kuwapeleka kwenye magereza ya nchi zao”
Mfungwa mwingine aitwae Ayowale ambae aliachiwa huru siku ya jumanne na kurudi Nigeria siku inayofata amekaririwa akisema “nilikwenda China mwaka 2004 kama mfanyabiashara ambae nanunua bidhaa huku na kuzituma nyumbani, 2006 nilikamatwa on charges of credit card fraud na nikahukumiwa jela miaka 10 mwezi march 2007″
Shuhuda mwingine ni Ejima ambae anasema alikwenda China 2006 na akakamatwa na kupelekwa gerezani november 2007 kwa kifungo cha miaka 7, ila ameachiwa huru miaka mitano baada ya kutumikia kifungo kwa sababu tu alikua anatumikia adhabu zake vizuri na kwa bidii”
Na Millard Ayo