Video Information
Frank Lampard akisherehekea bao lake
Jon Walters alifunga magoli
mawili katika lango na kupoteza mkwaju wa penalti huku Chelsea ikiilaza
Timu yake ya Stoke City kwa magoli 4-0.
Kufuatia ushindi huo Chelsea sasa imevunja
rekodi ya Stoke City ya kutoshindwa katika mechi yoyote katika uwanja
wao wa nyumbani.Kabla ya mechi hiyo Stoke ilikuwa imecheza mechi 17 katika uwanja wao bila kupoteza hata moja.
Walters aliifungia Chelsea bao la kwanza kwa kichwa baada ya Cesar Azpilicueta kupiga cross, na wakati alipokuwa akijaribu kuiondoa, kwa bahati mbaya likaingia ndani ya lango lao.
Dakika ya 45 kipindi cha kwanza Walters alifanya kosa kama hilo hilo na kufunga kwa mara nyingine kwa kichwa cross iliyopigwa na Juan Mata corner.
Frank Lampard naye akaifungia Chelsea bao la tatu kupitia kwa mkwaju wa penalti kabla ya Eden Hazard kufunga la nne kwa kombora alioupiga kwa zaidi ya mita 30 kutoka kwa goli.
Na kipindi hicho cha pili Stoke walipata penalti baada ya John Terry kumfanyia madhambi mchezaji wake lakini mkwaju wa
Walters uligonga mlingoti.
Matokeo mengine ya mechi za ligi kuu.
QPR 0 - 0 Tottenham
Aston Villa 0 - 1 Southampton
Everton 0 - 0 Swansea
Fulham 1 - 1 Wigan
Norwich 0 - 0 Newcastle
Reading 3 - 2 West Brom
Stoke 0 - 4 Chelsea
Sunderland 3 - 0 West Ham