Video Information
Rais Obama
Rais wa Marekani Barrack Obama,
amewataka wabunge wa bunge la wawakilishi kupitisha maazimio
yaliopitishwa na bunge la Senate kuhusu sera mpya ya uchumi bila kusita.
Bwana Obama, amesema kuwa makubaliano hayo
yanawaokoa asili mia sabini ya Wamarekani dhidi kupandishiwa ushuru na
pia yataimarisha uchumi uchumi waa taifa hilo.Rais Obama, amesema kuwa kwa mara ya kwanza wanaomiliki mabilioni na mamilioni ya fedha watalazimika kulipa ushuru unaohitajika kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka ishirini iliyopita.
Wabunge wa chama cha Republican, wamesema kuwa watahitaji muda zaidi kusoma mapendekezo hayo