Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

Mtuhumiwa ujambazi..

Views:
Video Information
JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro, linamshikilia mtuhumiwa wa mtandao wa uhalifu mkoani hapa,Abubakar Abdul(38), ambaye pia alikutwa na bastola pamoja na mtutu wa bunduki aina ya short gun kinyume cha sheria.
Kamanda wa polisi mkoni hapa,Ramadhani Mungi, amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa Machi 2 majira ya saa 6:00 mchana maeneo ya Kisangesangeni kata ya Kahe wilayani Moshi.
Amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa baada ya taarifa za siri kutoka kwa raia wema ambapo baada ya upekuzi alikutwa na bastola yenye namba ADP 0160A yenye risasi mbili pamoja na mtutu wa bunduki aliyokua amechimbia chini ya mti wa Mbuyu uliopo karibu na nyumbani kwake.
Kamanda Mungi amesema mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa ili kubainisha mtandao alionao katika kufanya matukio ya uhalifu wa kutumia silaha.
Katika tukio jingine polisi inawashikilia wakazi wa maeneo ya Rau na Majengo mjini Moshi, Philipo John(33) na Sisty Philipo(32) kwa tuhuma za kukutwa na lita 40 za pombe haramu ya Gongo pamoja na mitambo minne ya kutengeneza pombe hiyo.
Similar Videos