Video Information
Waziri wa mashauri ya nchi za nje
wa Rwanda amethibitisha kuwa
serikali inawafukuza maafisa sita
wa ubalozi wa Afrika Kusini, saa
chache baada ya Afrika Kusini
kuwataka raia watatu wa Rwanda
kuondoka nchini humo.
Afrika Kusini ilichukua hatua hiyo
baada ya nyumba ya mpinzani
mmoja wa Rwanda anayeishi Afrika
Kusini kushambiliwa siku ya
Jumaane.
Jenerali Kayumba Nyamwasa,
ambaye aliwahi kuwa mkuu wa
majeshi nchini Rwanda, hakuwa
nyumbani wakati wa shambulio
hilo.
Nyumba yake iliharibiwa na
komputa na baadhi ya nyaraka
zilichukuliwa.
Jenerali Nyamwasa amenusurika na
majaribio mawili mengine ya
kumuuwa akiwa Afrika Kusini.
Tayari watu wanafanyiwa kesi ya
kujaribu kumuuwa - wakiwemo
Wanyarwanda watatu na
Watanzania watatu.